Mzee Mtei afariki dunia, Rais Samia amlilia
- Amefariki dunia usiku wa kuamkia Januari 19, 2025, katika Jiji la Arusha.
Arusha. Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na mmoja wa waasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mzee Edwin Mtei, amefariki dunia usiku wa kuamkia Januari 19, 2025, katika Jiji la Arusha.
Taarifa za kifo hicho zilichapishwa kupitia chapisho lililotolewa katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter) na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John heche ambaye amesema kuwa chama hicho kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba huo.
“Tumepokea taarifa kwamba muasisi wa chama chetu, Mzee Edwin Mtei, amefariki dunia usiku wa leo tarehe 19/01/2025. Chama chetu kitatangaza taarifa rasmi kesho asubuhi,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Mzee Edwin Mtei aliwahi kuhudumu kama Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania kwa kipindi cha takribani miaka saba, kuanzia Juni mwaka 1966 hadi Januari 1974, akiacha alama muhimu katika historia ya sekta ya fedha na siasa nchini Tanzania.
Latest