Mvua kubwa yaja tena, TMA yatoa tahadhari ya siku mbili

October 16, 2019 7:04 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Mvua hiyo kubwa inaratajia kunyesha katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, visiwa vya Unguja na Pemba.
  • Mvua hiyo inatarajia kunyesha Oktoba 17 hadi 18, 2019
  • Changamoto zinazoweza kutokea ni pamoja na changamoto za usafiri na kusimama kwa baadhi ya shughuli za watu hasa za kiuchumi.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la mvua kubwa inayoweza kunyeshja katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya ukanda wa pwani ya kaskazini ikiwemo Dar es Salaam kwa siku mbili kuanzia kesho Oktoba 17

Angalizo hilo linahusisha mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Morogoro ambapo mvua kubwa za muda mfupi zinatarajiwa kunyesha.

Katika taarifa yake iliyotolewa jana (Oktoba 15, 2019), TMA imesema uwezekano wa kutokea kwa mvua hizo ni wa wastani na hata kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni cha wastani pia.

Mamlaka hiyo imeeleza baadhi ya changamoto zinazoweza kutokea ni pamoja na changamoto za usafiri na kusimama kwa baadhi ya shughuli za watu hasa za kiuchumi.

“Baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Mvua hizo kubwa za vipindi vifupi zinatarajiwa kunyesha kesho Oktaba 17 na 19.


Zinazohusiana


Hata hivyo, wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri kutoka TMA na kuzingatia tahadhari zilizotolewa na marejeo yake pamoja na kupata na kuzingatia ushauri na miongozo ya wataalam katika sekta husika ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV