Mufti Mkuu: Viongozi wa dini kemeeni mauaji ya kikatili

June 10, 2022 1:45 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni yanayohusisha watu waliopo kwenye mahusiano.
  • Ataka viongozi wa dini kuingilia kati. 

Dar es Salaam. Wakati matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo mauaji ya wanandoa yakiendelea kuripotiwa, Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakari Zuberi amekemea mauaji yanayoendelea nchini huku akiwataka watu kuzingatia mafundisho ya dini zao.

“Dini haitaki kuiua nafsi nyingine…kuua nafsi ni moja kati ya dhambi kubwa ambazo zitaangamiza watu wengi,” amesema Mufti Zuberi katika hafla ya uzinduzi wa Msikiti wa Masjid Jami’ ul Istiqama, uliozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, leo Juni10, 2022 Bukoba, mkoani Kagera.

Mufti Zuberi ametoa wito huo kufutia kuripotiwa kwa mauaji yanayoendelea nchini hasa yanayohusu wanandoa kuuana kwa wivu wa mapenzi.

Sambamba na kukemea vitendo vitendo hivyo, Mufti amesema Serikali peke yake haiwezi kumaliza suala hili la mauaji yanayoendelea kama  taasisi za kidini zIsipoingilia kati.

“Nyinyi kama Serikali kulisema likaisha hamuwezi lakini watu wa dini wanaweza kusema na watu wakasikiliza,” amesema Mufti Zuberi.


Soma zaidi: 


Katika hafla hiyo, Rais Samia amesisitiza masuala mbalimbali ikiwemo umuhimu wa chanjo ya Uviko-19, Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23 nchi nzima, akiwasisitiza viongozi wa dini zote kwenda kuhimiza suala la sensa kwa waumini wao.

“Sensa hata kwenye dini tunaitumia ili kujipanga vizuri na mambo yetu niwaombe sana Mashekh na viongozi muwahimize wananchi wakashiriki kikamilifu,” amesema Rais.

Rais Samia amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu iliyoanza tangu  Juni 8 mwaka huu ambapo akiwa mkoani humo alitembelea kiwanda cha Kagera Sukari na kuweka jiwe la msingi katika awamu ya tatu ya ujenzi wa kiwanda hicho.

Pia alizindua mradi wa maji wa Kyaka Bunazi  uliopo Wilaya ya Misenyi pamoja na kuzungumza na wananchi katika uwanja wa Kaitaba. 

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV