Mpango aagiza matumizi ya teknolojia kutathmini uharibifu wa misitu Tanzania

March 21, 2024 12:42 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Asema Teknolojia itasaidia kukabiliana na athari za ukataji miti nchini.
  • Aagiza ubunifu wa bidhaa mbadala za mitiikiwemo nishati za kupikia kupunguza uharibifu wa misitu kwa ajili ya kuni na mkaa.

Dar es Salaam. Makamu wa Rais Dk.Philip Isdory Mpango amegiza matumizi ya teknolojia katika kufanya tahmini ya uharibifu wa misitu ili kufahamu maeneo yaliyoathirika zaidi na jitihada zinazohitajika kukabiliana na tatizo la ukataji miti nchini.

Dk. Mipango ametoa maagizo hayo kwa Wizara ya Maliasili ya Utalii, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni (NCMC) Wakala wa huduma za Misitu (TFS) kwa kushirikiana na wadau wa misitu,  Machi 21, 2024 katika maadhimisho ya siku ya misitu Duniani yaliyofanyika Same, Kilimanjaro.

“Teknolojia hizo zitarahisisha ufuatiliaji na utoaji wa taarifa kwa kwa wakati kuhusu uharibifu wa misitu nchini,” amesema  Dk. Mpango.

Maagizo hayo ya Dk. Mpango yanakuja wakati ambapo Tanzania bado inakabiliwa na ukataji wa miti unaosababisha uharibifu wa misitu ya asili pamoja na ile ya kupandwa iliyopo nchini.


Soma zaidi:Wahitimu kidato cha nne 2023 ruksa kubadili tahasusi, chuo


Ripoti ya Utafii wa Athari za Upatikanaji wa Nishati Endelevu kwa mwaka 2021/2022 inayotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inabainisha kuwa asilimia 92 ya kaya zote Tanzania Bara hukata miti kwa ajili ya kuni na mkaa ambazo kuzitumia kama chanzo kikuu cha nishati kwa ajili ya kupikia.

Hiyo ni sawa na kusema kaya tisa kati ya 10 hukata miti kwa ajili ya kuni na mkaa huku asilimia 8.1 wakitumia nishati nyingine amboo zinatunza mazingira kupikia.

Aidha, Mpango amezitaka wizara, taasisi na wadau wa nishati Kubuni bidhaa mbadala wa zile zinazotokana na miti ikwemo zile zinazotumika kupikia kama nishati ya gesi ya kupikia (LPG) na mkaa mbadala.

“Jitihada hizi zijumuishe tafiti kuhusu nishati safi ya kupikia ya gharama nafuu, nishati mbadala ya kukausha tumbaku kwa mikoa inayolima tumbaku,” ameongeza Dk. Mpango.

Sambamba na maagizo hayo amewataka wakuu wa mikoa kuandaa programu zitakazosaidia kuongeza matumizi ya nishati safi za kupikia ambapo watatakiwa kutoa ripoti ya utekelezaji wa programu hizo kila baada ya miezi sita.

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Angela Kairuki amesema kila mwaka Tanzania hupoteza hekari 469 za misitu kutokana na  shughuli za binadamu pamoja na majanga asilia.

Kutokana na jambo hilo amewahamasisha Watanzania wote upanda au kutunza angalau miti mitano na kulinda misitu iliyopo kwa matumizi endelevu ya baadae.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW