Mbinu za kuthibitisha habari bila intaneti
- Ni pamoja na kusikiliza matangazo na habari kutoka mamlaka husika.

Arusha. Kuna namna nyingi za kuthibitisha habari zinazoweza kukusaidia kubaini ukweli hususani wakati huu tunapoelekea katika uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani unaotarajia kufanyika Octoba 29 mwaka huu.
Miongoni mwa namna hizo zipo ambazo hazihitaji matumizi ya intaneti zinazoweza kufanywa na wananchi wa kawaida wasiokuwa na simu janja au kompyuta ikiwemo kusikiliza matangazo na habari kutoka mamlaka husika.
Mbinu nyingine ni kuwahoji wataalamu au mashuhuda kupata taarifa za uhakika hasa zinazohusu uchaguzi, kusoma nyaraka au takwimu za mamlaka rasmi za Serikali au taasisi binafsi.
Pamoja na hizo, unaweza kusoma magazeti na majarida yenye vyanzo vya uhakika vya taarifa. Pamoja na hibitisha kwa kwenda eneo husika na kufanya uchunguzi wa moja kwa moja.
Latest



