Matumizi intaneti ya bure yashika kasi, wadau watoa neno

September 5, 2019 7:15 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Hadi mwaka 2018, watumiaji wa intaneti Tanzania wamefikia milioni 23.1 huku wanaotumia simu ni milioni 43.7.
  • Baadhi ya watu na makampuni yanatoa huduma za bure za intaneti ili kuchagiza biashara na uzalishaji.
  • Wadau wa teknolojia washauri mbinu mbadala za matumizi ya intaneti ya bure ili kulinda taarifa za watu mtandaoni.

Dar es Salaam. Matumizi ya intaneti nchini yanazidi kuongezeka ikizingatiwa kwamba watu wanaotumia simu janja wanazidi kuongezeka siku hadi siku.

Ripoti ya takwimu za mawasiliano za robo ya pili ya mwaka 2019 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonyesha kuwa Tanzania ina watumiaji wa simu za mkononi milioni 43.7 huku wanaotumia mtandaoni wa intaneti wakiwa ni milioni 23.1 sawa na asilimia 43 ya Watanzania.

Katika kuhakikisha intaneti inakuwa sehemu ya huduma muhimu kwenye jamii, wadau mbalimbali wanachagiza matumizi ya mtandao huo ikiwemo kujenga vituo vya kutolea huduma hiyo ili tu kuongeza kasi ya maendeleo.

Kampuni ya mtandao wa intaneti ya Liquid Telecom tayari imefungua vituo zaidi ya 150 vya intaneti ya bure katika maeneo mbalimbali nchini hasa katika migahawa inayowakutanisha watu kupata chakula na vinywaji.

Vituo hivyo pia vinapatikana katika majiji yote ya Tanzania ya Mbeya, Tanga, Mwanza, Arusha, Dodoma na Dar es Salaam ili kuwasaidia watu wasiopata intaneti kwenye simu au maeneo yao kuipata huduma hiyo bila malipo yoyote.

“Tumeanzisha vituo zaidi ya 150 vya intaneti ya bure kwenye majiji ya Tanzania. Hadi sasa zaidi ya watanzania 150,000 wanafurahia huduma za Raha za WI-FI (intaneti) ya bure,” amesema Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Tom Gutjahr.


Zinazohusiana:


Uwepo wa huduma hiyo una manufaa kwa watu ambao kazi zao zinahusisha mtandao kwani kupitia huduma hiyo, hawana hofu tena kwa sababu katika vituo hivyo inapatikana bure.

Huduma hiyo inaweza kuwasaidia watu kama Prosper Makundi ambaye ni mfanyabiashara anayesafiri mara kwa mara na  anategemea mtandao wa “WhatsApp” kufanya vikao kwa video na wafanyakazi wenzake.

“Niwapo Arusha, mtandao ninaotumia upo sawa. Kosa nikisafiri, wakati mwingine video call (upigaji simu wa video) ni changamoto kwa intaneti ya simu,” amesema Makundi.

Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Haji Said amesema huduma hiyo imeenea zaidi katika Jiji la Dar es Salaam kutokana na jiji hilo kuwa kitovu cha biashara na shughuli nyingi za uzalishaji mali.  

Said amesema, kwa kila kituo, kiwe kwenye migahawa na hata sehemu zingine, kinaweza kuhudumia watu 100 kwa wakati mmoja.

“Sehemu za vituo hivi zinachaguliwa kulingana na umaarufu na upatikanaji. Tunahitaji kuhakikisha kuwa kila mtu anafikiwa na huduma ya WI-FI,” amesema Said.

Kasi ya utoaji wa huduma hiyo, imeiwezesha kampuni hiyo kupata ugeni wa wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Columbia cha nchini Marekani ikiwa ni hatua ya kuonyesha namna kampuni hiyo imewezesha Tanzania kuendana na kasi ya kidigitali. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Liquid Telecom, Tom Gutjagr (katikati) akiwa na wageni kutoka Chuo Kikuu cha Columbia cha jiji la New York waliokuja kujifunza juu ya maendeleo ya kampuni hiyo katika kutoa huduma za mtandao wa intaneti kwa Watanzania. Picha| Liquid Telecom.

Uwepo wa huduma hiyo una manufaa kwa watu ambao kazi zao zinahusisha mtandao kwani kupitia huduma hiyo, hawana hofu tena kwa sababu katika vituo hivyo inapatikana bure. Picha|Mtandao. 

Intaneti hiyo ni salama?

Licha ya umuhimu wa intaneti ya bure, bado kumekuwa na maoni mchanganyiko juu ya matumizi yake, huku baadhi ya watu wakihofia usalama wa taarifa zao wakati wakitumia huduma hiyo.

Mtaalamu wa kujitegemea wa programu za kompyuta, Emmanuel Mtuchi amesema pale unapoomba kujiunga na mtandao wowote wa bure, inamwezesha mtoa huduma kuona vitu unavyovifanya mtandaoni.

Lakini Amesema watumiaji wa huduma hiyo hawapaswi kuhofia kwa sababu zipo njia mbalimbali za kujiweka salama wakati wakitumia intaneti ya bure ikiwemo teknolojia ya VPN (virtual private network) ambayo inasadia kuficha taarifa za mtu zisionekane kwa mtu mwingine asiyehusika.

Amesema watu wanaweza kuitumia intaneti hiyo kwa shughuli za kawaida kama kuperuzi mitandao ya kijamii lakini shughuli zinazohitaji umakini na usiri wa taarifa kama za benki na manunuzi ni vema wakatumia intaneti ambayo ni salama zaidi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV