Matinyi: mkopo wa Jamhuri ya Korea utalipwa kwa miaka 40

June 4, 2024 2:19 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Asema utaanza kulipwa kwa kipindi cha miaka 40 kuanzia mwaka 2028.
  • Ataja maeneo miradi mingine ambayo Jamhuri ya Korea inashirikianana Tnaznaia zinashirikiana kuitekeleza.

Dar es Salaam. Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi amesema mkopo wa Sh 6.5 trilioni uliikopwa na Serikali nchini Korea utalipwa kwa kipindi cha miaka 40 kuanzia mwaka 2028.

Kauli ya matinyi inakuja ikiwa imepita siku moja tangu rais Samia Suluhu Hassan na Rais Yoon Suk Yeol wa Jamhuri ya Korea washuhudie utiaji saini wa mkopo huo huku kukiibuka taarifa mbalimbali za upotoshaji kuhusu mkopo katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.

Taarifa hizo zinadai kuwa Serikali ya Tanzania imeweka rehani baadhi ya rasilimali ikwemo sehemu ya bahari na madini ili kukidhi vigezo vya kupewa mkopo huo jambo ambalo Matinyi amesema kuwa si kweli.

“Serikali yetu haijaweka rehani kitu chochote wala mali yoyote kama ambavyo imelezwa na baadhi ya vyombo vya habari…mkopo huu hauna masharti yoyote ya kuweka rehani kitu chochote,” amesisitiza Matinyi  wakati akizungumza na wanahabari leo Juni 4, 2024 jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wake mkopo huo kwa ajili ya miradi ya maendeleo una riba ya asilimia 0.01 ambayo inaufanya kuwa miongonni mwa mikopo nafuu ambayo Tanzania imewahi kukopa.

Msemaji huyo ameitaja mikopo mingine miwili ambayo nchi hiyo imewahi kuikopesha Tanzania ikiwemo wa Dola za Marekani milioni 733 (sawa na Sh1.9 trilioni) mwaka 2014 hadi 2020 na Dola za Marekani bilioni 1 (sawa na Sh2.6 trilioni) kati ya mwaka 2021 hadi 2025.


Soma zaidi: Jamhuri ya Korea kuikopesha Tanzania Sh 6.5 trilioni


Ni ushirikiano wa kimkakati

Mtinyi amewaambia wanahabari kuwa ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili ulioanza tangu mwaka 2014 ni wa kimkakati katika maeneo mbalimbali ikiwemo miradi ya maendeleo ambayo mingine tayari imeshafanyika.

Ameyataja maeneo hayo kuwa ni ujenzi wa Hospitali ya rufaa Mloganzila ambayo ni tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), awamu ya kwanza ya utoaji wa vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na utekelezaji wa mradi wa taka katika mkoa wa Iringa.

Miradi mingine ambayo ipo katika hatua ya utekelezaji ni pamoja na Ujenzi wa Bandari ya uvuvi Bagamoyo, ujenzi wa  kituo cha mikutano ya kimataifa Zanzibar, Ujenzi wa chuo cha tehama mkoani  Dodoma na mradi wa umwagiliaji visiwani Zanzibar.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV