Masharika yaliyositisha kutumia ndege za Boeing 737 Max 8 kulipwa matrilioni

July 23, 2019 3:57 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya kutokea kwa ajali za ndege mbili aina ya Boeing 737 Max za masharika ya Ethiopia na Indonesia. 
  • Haijataja idadi ya mashirika ya ndege yatakayopata fedha hizo.
  • Zaidi ya nchi 50 duniani zilisitisha kutumia ndege hizo kwa kuhofia usalama wa raia wake. 

Kampuni ya Boeing imesema italipa dola za Marekani  bilioni 4.9 sawa na takriban Sh11.3 trilioni kwa masharika ya ndege ambayo yalisimamisha safari zake baada ya ndege mbili aina ya Boeing 737 Max 8 kupata ajali na kuua watu 346. 

Ndege hizo zilikuwa zinamilikiwa na masharika ya ndege ya Ethiopia Airlines  na Indonesia (Lion Air) zilianguka kwa nyakati tofauti kutokana na hitilafu za kiufundi. 

Mataifa zaidi ya 50 ikiwemo China, Uingereza, India, Marekani  na Australia yalipiga marufuku mashirika ya ndani ya ndege ya nchi zao kutumia ndege hizo ikiwa ni hatua ya kuwalinda raia wao.

Katika taarifa yake iliyotolewa hivi karibuni, Boeing imesema kiasi hicho cha fedha  kitatumika kama fidia kwa masharika ya ndege ambayo yalisimamisha safari zake bila kuwa na ndege mbadala. 


Soma zaidi: 


Hata hivyo, kampuni hiyo ya Marekani haijaweka wazi idadi ya mashirika ya ndege yatakayopata fedha hizo huku ikijipanga kuwalipia fidia pia wateja ambao walipa usumbufu wakati ndege zake zilipositisha safari. 

Inaenelezwa kuwa baada ya majadiliano na marekebisho ya dosari kwenye ndege hizo, zingeweza kurudi tena kutoa huduma lakini Juni 26, mwaka huu, Mamlaka ya Anga la Marekani (FAA) ilitangaza kuwa imegundua kitu kingine kwenye ndege hizo na kuzizuia kuanza tena safari zake. 

Duru za habari za kimataifa zinaeleza kuwa ndege zaidi ya  370 aina ya Boeing 737 Max 8 zilizokuwa zinafanya safari maeneo mbalimbali duniani zilisitishwa baada ya mkasa wa ajali ya ndege ya hivi karibuni nchini Ethiopia.

Enable Notifications OK No thanks