Marekani yatafakari namna ya kutoa Sh3 trilioni kwa Tanzania

March 26, 2022 7:44 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya kupokea ombi la Tanzania ili izielekeze fedha hizo katika miradi ya kipaumbele.
  • Marekani imepanga kutoa fedha hizo kwa asasi za kiraia.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imeliomba Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) kuzielekezwa zaidi ya Sh3 trilioni katika miradi ya kipaumbele badala ya kuzipatia asasi za kiraia za Tanzania moja kwa moja.

USAID imepanga kutoa fedha hizo kwa asasi za kiraia katika kipindi cha miaka mitano ijayo ili kuimarisha utendaji na utekelezaji wa shughuli za kuwasaidia na kuboresha maisha ya wananchi. 

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba ametoa maombi hayo Machi 25, 2022 mkoani Dodoma, alipofanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi wa USAID, Kate Samvongsiri.

Dk Nchemba amesema ni kweli fedha hizo zina umuhimu katika miradi iliyokusudiwa kutekelezwa na asasi za kiraia lakini zielekezwe katika atika vipaumbele vya Samia Suluhu Hassan ikiwemo sekta za afya, elimu, kilimo, na zitakazochochea ukuaji wa uchumi.

“Tunapoandaa ushirikiano mpya na mipango mipya tunaomba mzingatie vipaumbele vya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambayo amewekeza nguvu kubwa, sambamba na yale mnayofanya kwenye sekta ya afya, elimu, kilimo, mazingira, pamoja na sekta zingine,” amesema Dk Mwigulu.

Amesema kwa sasa Rais Samia anajenga anatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na ameiomba USAID kuelekeza fedha hizo ambazo zinapitia kwenye mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), katika maeneo hayo.

 “Mfano, vituo vya afya vingi vimejengwa na watumishi wataajiriwa, mnaweza mkaweka nguvu kwenye vitendea kazi ambavyo bado havijakamilika ili huduma ziwe zinapatikana na lengo la Serikali pamoja na malengo mliyonayo ya kuendeleza huduma za jamii ambalo mnalo liweze kutimia,” amesema Mwigulu.

Tanzania na USAID zimekuwa na uhusiano wa zaidi ya miaka 50, na mwaka 2016, shirika hilo lilisaini mikataba mitatu ya msaada yenye thamani za zaidi ya Dola za Marekani milioni 635.5 (Sh1.5 trilioni), zilizotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii, programu ambayo itafikia tamati mwezi Septemba, 2022.

Mkurugenzi wa USAID, Kate Samvongsiri, amesema kuwa wanapenda kushirikiana na Serikali ya Tanzania na watakaa pamoja na kuangalia shughuli zinazofanyika katika sekta hizo za elimu, afya, kilimo, maji pamoja na zingine na kuona namna watakavyoziwezesha.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV