Mara, Dar zaibuka kidedea wanafunzi 10 bora matokeo darasa la saba

October 30, 2021 12:15 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Wanafunzi watano wanatokea shule ya Twiboki ya mkoani Mara.
  • Watano ni wavulana na watano ni wasichana.
  • Orodha nzima imebebwa na mkoa wa Mara na Dar es Salaam. 

Dar es Salaam. Mikoa ya Dar es Salaam na Mara imeibuka kidedea katika matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2021 baada ya wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri kitaifa kutoka katika mikoa hiyo pekee. 

Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Charles Msonde akitangaza matokeo hayo leo Oktoba 30, 2021 Jijini Dar es Salaam ametaja orodha ya wanafunzi 10 bora kuwa imetoka katika mikoa hiyo miwili tu.

Dk Msonde akitaja wanafunzi hao amesema nafasi ya 10 kitaifa  imeenda kwa Jackline Manfred kutoka Shule ya Msingi Masaka ya Jijini Dar es Salaam akifuatiwa na Juliana Shimbala wa Shule ya Msingi ya St Joseph ya Dar es Salaam.

Nafasi ya Nane imeenda kwa Rahma Juma kutoka Shule ya Msingi ya Mtuki Highland ya Dar es Salaam huku nafasi ya saba ikienda kwa Barnaba Magoto kutoka Shule ya Msingi ya Twibhoki ya Mkoani Mara.

Joctan Matara kutoka Shule ya Msingi ya Twibhoki ameshika nafasi ya sita na nafasi ya tano imechukuliwa na Eva Chengula kutoka Shule ya Msingi ya Fount of Joy ya Dar es Salaam.

Nafasi ya nne ni yake Joshua Jacob, wa tatu ni John Charles na wa pili ni Happy Deus wote kutoka Twibhoki.

Nafasi ya kwanza imeenda kwa Eluleki Haule kutoka Shule ya Msingi ya St Anne Marie ya jijini Dar es Salaam. 

Kati ya watahiniwa hao, watahiniwa watano sawa na silimia 50 ya orodha hiyo wanatoka Shule ya Msingi ya Twibhoki ya mkoani Mara. 

Pia katika mchuano huo wa 10 bora kitaifa, ina mgawanyo sawa wa kijinsia ambapo wavulana ni watano na wasichana ni watano. 

Katibu Mtendaji wa Necta,  Dk Charles Msonde amesema watahiniwa bora kitaifa ni wale ambao wamepata alama nyingi zaidi kuliko wengine kwenye masomo sita waliyofanyia mtihani.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV