Mapato ya dhahabu iliyouzwa nje ya nchi yaongezeka kwa asilimia 45.5 Tanzania

February 13, 2020 6:58 am · Nuzulack Dausen
Share
Tweet
Copy Link
  • Ongezeko hilo la mapato hayo ya dhahabu limechangiwa zaidi na kupaa kwa kiwango cha madini yaliyouzwa nje ya nchi na kuongezeka kwa bei katika soko la dunia.

Dar es Salaam. Mapato ya mauzo ya dhahabu nje ya nchi yameongezeka kwa asilimia 45.5 ndani ya mwaka mmoja yakichagizwa zaidi na kupaa kwa kiwango cha shehena iliyouzwa pamoja na bei katika soko la dunia.

Ripoti mpya ya mapitio ya uchumi ya Januari 2020 (Monthly Economic Review)  ya  Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inabainisha kuwa mapato ya dhahabu iliyouzwa nje ya nchi yaliongezeka hadi Dola za Marekani 2.22 bilioni (Sh5.08 trilioni) mwaka 2019 kutoka Dola za Marekani 1.52 bilioni (Sh3.5 trilioni) mwaka 2018.

“Mauzo ya dhahabu nje ya nchi, ambayo ni asilimia 52.3 ya bidhaa zisizokuwa za mazao (non-traditional exports), yaliongezeka kwa asilimia 45.5 hadi Dola za Marekani 2.217 bilioni (Sh5.08 trilioni), yakichagizwa na kuongezeka kwa kiwango na bei katika soko la dunia,” imesema ripoti hiyo ya BoT iliyotolewa mapema wiki hii.



Hata hivyo, benki hiyo haikubainisha kiwango cha shehena ya dhahabu iliyouzwa nje ya nchi mwaka jana.

Serikali ya Rais John Magufuli imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuongeza faida za madini Tanzania ikiwemo kubadili sheria na kanuni zinazoziba mianya ya rasilimali hizo kutoweshwa kirahisi nje ya nchi bila kulipa kodi stahiki.

Mapema mwaka jana, Serikali ilianzisha masoko ya madini katika kila mkoa wenye rasilimali hizo ili kuboresha ukusanyaji imara wa taarifa za uzalishaji madini na mapato ya Serikali.

Katika ripoti hiyo, BoT imesema mapato ya jumla ya uuzaji wa bidhaa na huduma nje ya nchi yaliongezeka hadi Dola za Marekani 9.71 bilioni (Sh22.24 trilioni) mwaka 2019 kutoka Dola za Marekani 8.39 bilioni (Sh19.22 trilioni) mwaka juzi.

“Katika miezi ya hivi karibuni, hali iliimarika zaidi kutokana na kuongezeka kwa mapato yatokanayo na huduma na thamani ya bidhaa zisizo za mazao,” imesema BoT.

Dhahabu ni moja ya vyanzo vikubwa vya fedha za kigeni nchini Tanzania sanjari na utalii. Picha|Wikiendi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV