Mapato ya Apple, Amazon yapaa

July 29, 2022 11:29 am · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Mapato ya Apple yapanda kwa asilimia 2 robo ya tatu ya 2022.
  • Amazon mapato yake yaongezeka kwa asilimia 7.
  • Ni kutokana kuongezeka kwa bidhaa za kampuni hiyo.

Kampuni ya teknolojia na vifaa vifaa vya kielektroniki ikiwemo simu ya Apple imesema mauzo ya bidhaa na huduma zake yameongezeka kwa asilimia mbili hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 83 sawa na Sh 193.5 trilioni katika robo ya tatu ya mwaka 2022. 

Afisa Mkuu wa Fedha wa kampuni hiyo inayotengeneza simu za iPhone,  Luca Maestri katika taarifa yake ya Julai 28, 2022  amesema wamepta mafanikio hayo katika kipindi ambacho nchi nyingi duniani zinakumbana na changamoto za kushuka kwa uchumi na athari ya mgogoro wa vita ya Urusi na Ukraine.

Simu na huduma za Iphone zimeendelea kuwa na hitaji kubwa kwa wateja huku huduma za malipo (Apple Pay) na mauzo ya muziki mtandaoni (iTunes) yakiongezeka kwa asilimia 12 ikilinganishwa na ripoti ya awali.

Pia kampuni ya Amazon inayoshughulika na biashara za mtandaoni, uchukuzi wa kidijitali imeripoti ongezeko la mapato kwa asilimia 7 kufikia Dola za Marekani bilioni 121.2 sawa na Sh282.1 trilioni ingawa mauzo ya mtandaoni yamepungua kwa asilimia 4 kwa mwaka.

Amazon imeendelea kupata faida kupitia ya asilimia 33 ya mauzo ya huduma za mtandao (AWS), komputa anga (cloud computing division) na akili bandia (Artificial Intelligence)

“Licha kuendelea kupanda kwa gharama za mafuta, nishati na gharama za usafirishaji, tunapiga hatua zaidi kwenye gharama zinazoweza kudhibitika hasa katika kuboresha mtandao wa utimilifu” alisema Andy Jassy afisa mtendaji wa Amazon.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV