Mambo yatakayowasaidia wanafunzi wa sheria kufaulu mitihani

October 15, 2022 11:04 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Wadau wavishauri vyuo vya sheria kuweka nguvu kwenye vitendo na sio maneno.
  • Wasema kutofanya vitendo ni miongoni mwa sababu ya wanafunzi kufeli shule ya sheria kwa vitendo. 

Dar es salaam. Wadau wa masuala ya sheria nchini Tanzania wameishauri Serikali na taasisi zinazofundisha kozi za sheria kuweka nguvu kwenye mafunzo kwa vitendo zaidi kuliko nadharia ili kuwawezesha wahitimu kupata ujuzi utakaowasaidia baada ya kumaliza masomo.

Ushauri huo unakuja zikiwa zimepita siku chache tangu matokeo ya mtihani wa Shule ya Sheria kwa Vitendo (LST) kwa mwaka 2022  kuonyesha ni wanafunzi 26 pekee kati ya 633 waliofaulu mtihani. 265 kati yao walifeli na kuondolewa masomoni (discontinue)  na 342 wakitakiwa kurudia mitihani (supplementary).

Edward Heche ambaye ni Mwenyekiti wa Wanasheria Vijana kutoka Chama Cha Mawakili Tanganyika (TLS) aliyekuwa akiongea wakati wa ufunguzi wa mashindano ya uanasheria kwa vitendo (moot court ) leo Oktoba 15, 2022 jijini Dar es Salaam amesema taasisi zinazotoa taaluma ya sheria zinapaswa kubadili mitaala kutoka kuwa ya nadharia na kuwa vitendo zaidi.

“Ni lazima kuwe na mabadiliko katika mfumo wetu wa elimu, katika miaka mitatu au minne kuwe na miaka miwili ya kujifunza kwa vitendo kabla ya kwenda shule ya sheria, muda wa kukaa shule ya sheria ni mdogo kwa mtu kujifunza vitu vyote kwa vitendo,” amesema Heche.


Soma zaidi:


Kwa upande wake Wakili  Benedict Ishabakaki ambaye ni miongoni mwa waandaji wa mashindano hayo amesema lengo lao ni kuimarisha sekta ya sheria kwa kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi juu ya nini wanapaswa kufanya katika taaluma hiyo.

“Lengo kuu ni kujengea wanafunzi uwezo wa kusimamia sheria kwa vitendo, tunakusanya wanafunzi Tanzania nzima tunawapa swali la mtego halafu wanakuja mbele ya majaji ambao ni mawakili ambao watawapima,” amesema Ishabakali 

Mashindano hayo yanafanyika, ukiwa ni msimu wake wa pili ambapo jumla ya wanafunzi 20 kutoka vyuo mbalimbali vinavyofundisha sheria hushindanishwa kwa kupimwa ujuzi wa sheria kwa vitendo.

Hupewa ushauri kutoka kwa mawakili ambapo kwa mwaka huu mashindano hayo yanaangazia dhima ya utunzaji faragha.

Washiriki wanasemaje

Catherine Oscar Michael ni mwanafunzi wa shule ya sheria kwa vitendo amesema kwa upande wake mashindano hayo ni muhimu kwani mafunzo kwa vitendo ndiyo msingi wa utekelezaji wa majukumu yao.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV