Makala kuenzi utendaji kazi wa Makonda, Kenani Arusha

August 29, 2025 5:58 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Aahidi kufanya ziara kila kata kutatua changamoto za wananchi

Arusha. Mkuu wa Mkoa wa mpya wa Arusha Amosi Makala, ameahidi kusikiliza kero za wananchi katika kila kata kama ilivyokuwa ikifanyika na watangulizi wake Paul Makonda pamoja na Kenani Kihongosi.

Agosti 23 mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan alimteua Makala kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha akimrithi Kenani Kihongosi aliyeongoza jiji hilo kwa miezi miwili.

Makala ametoa ahadi hiyo alipokuwa akipokelewa rasmi katika ofisi za mkuu wa mkoa jijini humo leo Agosti 29, 2025 akisisitiza kuwa atawatumikia wananchi kwa kuwafuata katika kata na wilaya zao na kutatua kero zilizopo.

“Nitawafuata mlipo wale wanaodhani wakija kwa Mkuu wa Mkoa mara kwa mara watanikuta ofisini siyo hiyo….mimi napenda kufanya kazi na wananchi tunataka kuwasikiliza wananchi tunataka kutatua kero za wananchi,” amesema Makala.

Aina hiyo ya utendaji kazi ya kusikiliza kero za wananchi iliwahi kufanywa na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda ambaye kwa sasa ni mgombea ubunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuendelezwa na Kenani Kihongosi.

Makala amebainisha kuwa ziara ayake ya kwanza itakuwa katika Wilaya ya Ngorongoro ambayo kwa mujibu wake viongozi wengi walikuwa hawafiki mara kwa mara.

Aidha, Makala amewataka wananchi wa mkoa huo kudumisha amani ili kuendelea kuvutia utalii ambao ni kitovu cha uchumi wa jiji hilo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV