Majaliwa ataja manufaa ya mpango kabambe wa uvuvi

September 20, 2022 2:06 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Utasaidia kukuza sekta hiyo na kuongeza mchango wake katika pato la Taifa hadi kufikia asilimia 10 kwa mwaka kutoka asilimia 1.8 ya sasa.  

Dar es Salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Sekta ya Uvuvi utasaidia kukuza sekta hiyo na kuongeza mchango wake katika pato la Taifa hadi kufikia asilimia 10 kwa mwaka kutoka asilimia 1.8 ya sasa.  

Majaliwa amesema kuwa mpango huo ambao utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka 15 kuanzia 2021/22 hadi 2036/37 una umuhimu mkubwa  katika ukuaji wa sekta ya uvuvi pamoja na uchumi wa buluu.  

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwahakikishia wadau wote wa sekta ya uvuvi kuwa Serikali ina nia ya dhati ya kuhakikisha kila mmoja ananufaika na sekta hiyo. 

Amesema hayo leo Septemba 20, 2022 wakati wa uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Sekta ya Uvuvi, katika ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jijini Dar es Salaam.  

“Tutaendelea kupokea mapendekezo yenu ili tuweze kuboresha sekta hii, ubunifu wenu ni muhimu, wote tunataka tuzungumze lugha moja,” amesema Majaliwa.

                     

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
NISHATI

NISHATI

Nukta TV

Utani wa Rais Samia kwa wachimba madini wa Katoro

Utani wa Rais Samia kwa wachimba madini wa Katoro

Nukta TV

Rais Samia: Misaada imepungua, tukaze buti

Rais Samia: Misaada imepungua, tukaze buti

Nukta TV