Mafundi sanifu, michundo kupigwa msasa zaidi

May 24, 2019 3:34 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB), Professa Ninatubu Lema, amesema kuwa wasanifu majengo wanahitajika kujituma ili kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya kutengeneza bidhaa mbalimbali. Picha|Mtandao.


  • Serikali imesema inaratibu mafunzo ya kuwajengea uwezo ili kuongeza idadi ya wataalam hao.
  • Itawahusisha katika miradi ya ujenzi wa miundombinu ya reli ya kisasa (SGR) na daraja la Selander.
  • Pia kupelekwa nje ya nchi kujifunza ujenzi wa viwanda vidogo vidogo.

Dar es Salaam. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imesema itaendelea kuwajengea uwezo na uzoefu mafundi sanifu na mafundi michundo kuwawezesha kutekeleza kazi zao kwa ufanisi na kuziba pengo la wataalam hao katika katika sekta ya ujenzi. 

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Elius Mwakalinga aliyekuwa akizungumza  jijini Dar es Salaam katika mkutano wa wasanifu majengo na mafundi michundo, amesema kuwa Serikali imejikita katika kuhakikisha sekta ya ujenzi wa miundombinu hasa majengo inafanikiwa kwa kuwa na watalaam wengi wenye weledi.

“Serikali imedhamiria kujenga miundombinu ili kuwezesha ukuaji wa sekta ya Viwanda nchini, hivyo mafundi sanifu wanategemewa sana katika kuwezesha miundombinu hii, ili Tanzania iweze kufikia ndoto ya kuwa kwenye uchumi wa kati kupitia viwanda.

“Katika kutekeleza hilo mwaka wa fedha 2019/2020, Wizara ya Ujenzi imejikita katika ajenda tatu ikiwemo kuwajengea uwezo wasanifu na wahandisi wote nchini,” amesema Dk Mwakalinga.


Soma zaidi:


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari Maelezo leo, Serikali itahakikisha watalaam chini ya taaluma ya uhandisi, usanifu majengo, ukadiriaji majenzi wanaongezeka kiidadi na kujengewa ujuzi mahususi ili kuwa na uwezo wa kumudu mahitaji ya nchi.

Katika kufanikisha hilo, kuanzia Julai Mosi mwaka huu, Serikali kwa kushirikiana na bodi mbalimbali za taaluma za kihandisi wataanza kuwaweka wataalam hao katika miradi inayotekelezwa nchini ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), ujenzi wa ‘Interchange’ ya Ubungo, ujenzi wa bwawa kubwa la kuzalisha umeme mto Rufiji na ujenzi wa daraja la Selander ili wapate uzoefu.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB), Professa Ninatubu Lema, amesema kuwa wasanifu majengo wanahitajika kujituma ili kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya kutengeneza bidhaa mbalimbali.

Amesema wanaangalia namna ya kwenda kujifunza katika nchi za China na India jinsi mafundi wao wanavyohusika katika ujenzi wa viwanda vidogo ili kuwaongezea maarifa wataalam wa Tanzania. 

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW