Madhara ya corona: UNICEF yaangazia namna ya kuwarudisha wanafunzi shuleni

May 5, 2020 12:06 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Imesema wanafunzi waliopo vijijini hawapati fursa ya kujifunza.
  • Yaandaa mwongozo utakaotumika kuwarudisha wanafunzi shuleni.

Dar es Salaam. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) limeeleza kuwa linaangalia uwezekano wa kufungua shule katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika ambako wanafunzi wengi hawapati fursa ya kusoma kutokana na janga la Corona.

Janga hilo limewaathiri zaidi watoto waishio vijijini ambao wanakabiliwa na changamoto ya kukosa umeme na intaneti, licha ya Serikali za nchi hizo kuanzisha utaratibu wa kusoma kwa njia ya redio na mtandaoni. 

UNICEF katika taarifa yake iliyotolewa Mei 4 nchini Kenya na Afrika Kusini, imeeleza kuwa zaidi ya watoto milioni 127 wa shule za awali, msingi na sekondari katika nchi hizo wataendelea kukaa nyumbani kutokana na kutotengamaa kwa hali ya virusi vya COVID-19.

“Katika maeneo mengi ya dunia, kujifunzia nyumbani kumesaidiwa na zana za mtandaoni. Hata hivyo, katika maeneo ya Afrika Mashariki na Kusini, kupenya au kusambaa kwa intaneti ni kugumu, ambapo ni kaya moja tu kati ya tano sawa na asilimia 22 ambao wana intaneti, wakati asilimia 84 ya watu wa vijijini ambako idadi kubwa ya wanafunzi wanapatikana, hawana umeme,” imeeleza taarifa hiyo.

Katika Kushughulikia sintofahamu hiyo, UNICEF imetangaza usaidizi zaidi kwa janga hili la elimu ambalo halijawahi kutokea, wakati ikiendelea kutafuta namna ya ufunguzi wa shule unaozingatia mwongozo wa usalama.


Zinazohusiana


UNICEF imeandaa mwongozo mpya wa kiufundi uliopewa jina “Mfumo wa kufungua Shule” ambao unatoa muundo wa kufungua upya shule ili kuwapa fursa ya kusoma wanafunzi ambao hawawezi kujifunza kwa njia ya mtandao au redio.

Mwongozo huo uliandaliwa kwa ushirikiano wa Shirika la Mpango wa Chakula (WFP), Benki ya Dunia, Shirika la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO na UNICEF yenyewe.

Hata hivyo, haijaweka bayana ni lini wanatarajia mpango huo utaanza kutekelezwa.

Mpaka sasa shirika hilo limezisaidia Serikali za nchi hizo zaidi ya dola milioni 5.4 (Sh12.5 bilioni) kwa ajili ya masomo na pia kwa ajili ya maandalizi ya kuzifungua shule huku ufadhili zaidi ukiwa katika mipango.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Nukta TV

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Nukta TV

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Nukta TV