Lissu: Kuna mapungufu katika ushahidi, hati ya mashtaka

September 24, 2026 6:44 pm · Method Allen
Share
Tweet
Copy Link
  • Asema kuna mapungufu katika ushahidi, sheria na hati ya mashtaka
  • Kesi itaendelea tena kesho Septemba 25, 2026.

Dar es Salaam. Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, imeendelea leo Septemba 24, 2026, huku akiendelea kuwasilisha hoja zake za mwisho ili kuishawishi mahakama kuwa hana hatia.

Lissu anayeshtakiwa kwa kosa la uhaini kinyume na Sheria ya Kanuni ya Adhabu iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2023 linalotokana na tuhuma za matamshi aliyoyatoa Aprili 3, 2025 jijini Dar es Salaam ya kutoshiriki na kuzuia Uchaguzi Mkuu 2025 ametumia saa tisa kuilezea mahakama kuwa hana hatia kwa mujibu wa sheria.

“Haya matendo ambayo nimeshitakiwa nayo, hayakai sehemu ya matendo kumi yaliyotajwa kuwa ni makosa ya uhaini, maana yake ni kwamba mimi sijafanya kosa lolote la uhaini.

Kama sijafanya kosa la uhaini, je nimefanya kosa lingine lolote kwa mujibu wa Sheria ya Tanzania?,” amehoji Lissu mbele ya majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam wanaoendesha kesi hiyo.

Mapungufu katika ushahidi

Katika hoja zake leo Lissu amebainisha mapungufu katika ushahidi uliotolewa na mashahidi watatu upande wa mashtaka.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameendelea kujitetea katika kesi ya uhaini inayoendelea katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ndogo ya Dar es Salaam | Picha Method Allen

Mashahidi hao ni PW1, PW2 na PW16 ambao wote ni askari polisi waliotoa ushahidi wao mwishoni mwa mwezi Agosti, 2026 akidai kuwa ushahidi wao unafanana hivyo hauna mashiko na una mikanganyiko na kwamba wote hawajathibitisha yeye kuitisha mkutano na kusema maneno yanayodaiwa kuwa uhaini.

Maneno pekee hayawezi kuwa “tendo” la uhaini

Hoja nyingine ya Lissu imepinga tafsiri ya upande wa mashtaka kwamba maneno aliyoyasema yanaweza kuchukuliwa kama “overt act” (tendo la bayana) katika kosa la uhaini.

Amesema sheria inahitaji kuwepo kwa kitendo bayana kinachoonyesha nia, hivyo maneno yaliyosemwa hayawezi kubadilishwa kuwa tendo kwa tafsiri ya upande wa mashtaka.

Kiongozi huyo wa upinzani pia amehoji matumizi ya neno “altering” katika hati ya mashtaka, akisema katika Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code, Cap. 16) neno hilo linahusishwa na makosa kama forgery (kughushi nyaraka) na kubadilisha nyaraka, si kitendo cha kubadilisha au kutamka maneno kama kinavyoelezwa katika shtaka dhidi yake.

Dosari katika hati ya mashaka
Kwa mujibu wa Lissu, hati ya mashtaka imetumia maneno ambayo kwa mtazamo wake hayana msingi katika kifungu cha sheria anachotuhumiwa kukikiuka, hivyo shtaka hilo ni lenye kasoro isiyoweza kurekebishika na haliwezi kutibika.

“Hati ya mashtaka ni batili…imetaja kitu ambacho hakipo kwenye sheria.” amesisitiza Lissu.

Kutokana na ufinyu wa muda Mahakama imeamuru Lissu kuendelea kufanya majumuishi ya hoja zake kesho Septemba 25, 2026 saa tatu asubuhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Oct, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
18 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
18 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mambo ya kuzingatia unapoanzisha chombo cha habari mtandaoni (ONLINE MEDIA)

Mambo ya kuzingatia unapoanzisha chombo cha habari mtandaoni (ONLINE MEDIA)

Nukta TV

HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

Nukta TV

TBS yatoa tahadhari matumizi ya ‘sponge’ kupika chapati

TBS yatoa tahadhari matumizi ya ‘sponge’ kupika chapati

Nukta TV