“Last blood”, “Abominable” kutikisa hisia za wapenda filamu wiki hii

September 27, 2019 9:20 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Licha ya kuibua hisia kwa mtazamaji, filamu hizi zitakufundisha kuwa binadamu mwema ana mapenzi na familia yake. 
  • Zinaonyeshwa kwa siku saba kuanzia leo Septemba 27 katika kumbi mbalimbali za sinema.

Dar es Salaam. “Kwanini niangalie filamu?” Unaweza ukajiuliza hili swali ukidhani hakuna lolote unalopata kutokana na kuangalia filamu. 

Ukweli ni kuwa, mbali na burudani, kuna mambo mengi yaliyojificha nyuma ya utazamaji wa filamu.

Kabla sijakupeleka kwenye filamu za kuangalia wiki hii, ni vyema ukafahamu kuwa unapocheka wakati unaangalia filamu ya kuchekesha, unachochea mzunguko mzuri wa damu.

Zaidi, kuangalia filamu ya kutisha kwa masaa mawili inaunguza kalori “calories” 113 ambayo ni sawa na zoezi la kutembea kwa dakika 30.

Baada ya kufahamu tone la faida lukuki za kutazama filamu, una kila sababu ya kutembelea kumbi za kuangalizia filamu zikiwemo Mkuki House, Mlimani City na Dar Free Market kwa siku saba kuanzia leo (Septemba 27, 2019) kuangalia filamu zilizoingia sokoni. 

Filamu ambazo zitaonyeshwa katika kumbi hizo hasa kwa wakazi wa Jijini Dar es Salaam ni pamoja na:

Rambo 5: Last Blood

Chini ya muongoza filamu Adrian Grunberg,  John Rambo (Sylvester Stallone) ambaye ni mkongwe wa vita za Vietnam yupo kwenye hali shwari nyumbani kwake Arizona. 

Tafrani inaanza pale Hugo Martinez (Sergio Peris-Mencheta) anapomteka Gabriela (Yvette Monreal) alipoenda kutafuta ukweli kuhusu baba yake. 

Rambo ni kati ya filamu zilizoongelewa sana hapo zamani. muendelezo huu ni kumbukumbu za enzi zetu” amesema Christian Kulwa ambaye ni shabiki wa filamu. Picha| Mtandao.

Anachokitaka Rambo ni Hugo amrudishe Gabriela ambaye ni kati ya watu wake wa karibu (familia) lakini pale hitaji hilo linaposhindwa kufikiwa ndipo vita kati ya wawili hao inapoanza. Ni vita ya mtu mmoja dhidi ya makumi ya watu. 

Una kila sababu ya kufuatilia vita hii kati ya mkongwe(Veteran) wa vita dhidi ya mafia mwenye ujanja na watu lukuki. Nani atabaki anasimama? Jibu swali hilo utalipata kwenye filamu hiyo iliyogharimu Sh114.9 bilioni.


Zinazohusiana


Abominable

Kumbi za filamu wiki hii pia hazijaacha kuweka nafasi kwa ajili ya watoto kwani simulizi ya Abominable inayomhusu Yi (Chloe Bennet) ambaye anagundua uwepo wa “Yeti” (kiumbe anayesadikika kuishi kwenye milima Himalaya) juu ya Ghorofa la nyumba anayoishi.

Baada ya kumbatiza Yeti  jina la Evarest, Yi anaungana na marafiki zake kumpeleka Everest kwenye shehemu ya juu zaidi duniani ili Everest aungane na familia yake.

Je, kwa vikwazo ambavyo vinawasubiri njiani watafanikisha safari yao, licha ya kuibua hisia kwa mtazamaji, filamu hii itakufundisha kuwa binadamu mwema.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW