Kwaheri: Necta yafuta orodha ya 10 bora kidato cha nne Tanzania

January 31, 2023 11:53 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Bosi wa Necta amesema utaratibu huo hauna tija na huenda baraza lilikuwa linawafanyia watu matangazo bila kujua.
  • Baadhi ya wadau wapongeza uamuzi huo wa baraza wakieleza kuwa utasaidia kupunguza wizi wa mitihani.

Dar es Salaam. Wazazi na viongozi wa shule waliokuwa wakisubiri kwa hamu kuona iwapo watoto wao wameingia katika orodha ya dhahabu ya 10 bora katika mitihani ya taifa sasa watasubiri sana jambo hilo baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) kutangaza kufuta rasmi utaratibu huo likisema “hauna tija”.

Uamuzi wa Necta kufuta utaratibu huo uliokuwa ukishindanisha wanafunzi, shule, wilaya na mikoa kupitia orodha ya 10 bora huenda ukapeleka maumivu kwa baadhi ya viongozi waliokuwa wanatumia takwimu hizo kuvuta zaidi wanafunzi au kuonyesha ubora wa utendaji kazi wao.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta Athuman Amas amewaambia wanahabari sasa baraza hilo limeuondoa utaratibu huo ambao hata wanahabari waliokuwa ndani ya chumba cha mikutano walikuwa wakisubiri kwa hamu kujua nani ni nani.

“Tumeondoa utaratibu wa kutangaza shule 10 bora au watahiniwa 10 bora kwa sababu hauna tija, tunawafananisha watu ambao wamefanya mtihani sawa lakini mazingira tofauti,” amesema Amas huku baadhi ya wanahabari wakionekana kukubaliana na uamuzi huo.

Kwa miongo kadhaa sasa Necta imekuwa ikishindanisha shule 10 bora kitaifa na wanafunzi 10 bora huku yule wa kwanza maarufu kama “Tanzania One” (TO) akipewa heshima zaidi.

Baadhi ya shule hizo hasa binafsi na za mashirika ya dini zimekuwa zikitumia orodha hiyo kwenye matangazo ya biashara kuvutia wazazi kupeleka watoto kwenye taasisi zao huku baadhi zikihusisha mchujo mkali.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athuman Amas akiwasilisha matokeo ya kidato cha nne na mtihani wa maarifa (QT) mwaka 2022 kwa wanahabari jijini Dar es Salaam Januari 29, 2023. Picha|Esau Ng’umbi/Nukta. 

“Unamtaja huyo mtu kwamba ameongoza katika kundi ambalo pamoja na kuwa wamefanya mtihani mmoja lakini hawakusoma katika mazingira yanayofanana, wakati mwingine niseme tu kutangaza shule ya kwanza, inawezekana kama mheshimiwa mwandishi ulikuwa na shule, huenda tulikuwa tunakufanyia matangazo, huenda nasema,” amesema Amas huku wanahabari wakiangua kicheko.


Zinazohusiana: 


Mara baada ya kutangazwa uamuzi huo, baadhi ya wadau wa elimu wamefurahia uamuzi huo wa Necta huku wengine wakishauri kuwa ili orodha hiyo iwe ina maana Serikali inapaswa kuboresha mazingira ya kijifunzia katika shule zote.  

Mtumiaji wa mtandao wa Twitter Herr Kidori @SamGidori amesema ikipendeza Necta wafanya uamuzi huo wa kufuta orodha ya 10 bora na kwa kidato cha sita pia.

Mdau mwingine wa Twitter ajulikanaye kama @Suahibu_ amesema ili kuondoa utofauti huo ni vyema Necta ikatoa orodha ya 10 bora kwa shule za umma na shule binafsi. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV