KANUNI YA 5: Mazoezi hayana mbadala kwa afya bora
Mazoezi ni muhimu sana. Anza taratibu kwa kutembea walau dakika kumi. Hakuna ubize wowote au majukumu yanayokunyima hata dakika 20 za muda huru. Picha|Fitsum Admasu /Unsplash.
- Mazoezi huimarisha uwezo wa ubongo kufanya kazi.
- Huondoa msongo wa mawazo na kukupa muonekano mzuri wa nje.
- Tenga walau dakika 10 hadi 30 za mazoezi kila siku.
Unahitaji kuwa na ufanisi zaidi kazini? Je unataka kufanya vizuri unapokuwa na mwenza wako au mpenzi wako? Kama majibu yako kwa maswali haya ni ndiyo, basi mazoezi ndio suluhisho kwa haya yote.
Zoezi ni aina yoyote ya shughuli yenye kupangiliwa kwa muda, lengo ni kuwa na matokeo maalum katika mwili wako. Kuna watu hufanya kazi  ngumu kisha wakasema hilo ni zoezi tosha. La hasha!.Â
Kazi unayofanya siyo mazoezi, bali ni sehemu ya majukumu yako ya kila siku. Hivyo basi hata wewe unahitaji aina fulani ya mazoezi ili uwe imara na kuimarika. Je una sababu gani ya kufanya mazoezi? Kwanini ni kanuni muhimu ya afya?
Mazoezi huimarisha uwezo wa ubongo kufanya kazi. Mazoezi siyo tu huimarisha mwili bali hata ubongo. Wale walio na tabia ya kufanya mazoezi hata utendaji wao tu kazini ni tofauti. Ufanisi na utendaji wa kazi hu ni bora Zaidi. Na hii sio tu kwa walio ajiriwa bali hatawenye ajira zao.Â
Mazoezi huyeyusha msongo na mkazo. Kufanya mazoezi hukupa hali ya kutulia ambayo huleta mtazamo chanya. Hii huimarisha hali yako ya nje na kukuondolea msongo wa mawazo.Â
Unapokuwa huna msongo wala mkazo ni ngumu kukwazika bila sababu au kukasirika. Hii itaimarisha mahusiano yako na watu wanaokuzunguka ikiwemo wafanyakazi, familia pamoja na marafiki.
Mazoezi hukuongezea nguvu. Kukimbia kwa takribani dakika 30 hufanya homoni za endorphin ziachiliwe na kukufanya ujisikie mwenye nguvu baada ya mazoezi hayo.
Huimarisha stamina na unapokua na nguvu basi hata utimilifu wako katika majukumu unakua ni mkubwa ukilinganisha na ukiwa hufanyi mazoezi.
Zinazohusiana:
- Jinsi unavyoweza kuishinda sonona isiharibu maisha binafsi, kazi
- Mambo yatakayokusaidia kupunguza hatari ya kupata sarataniÂ
- Fanya haya kulinda afya kazini
Unajua mazoezi yanaimarisha mahusiano?
Tafakari unapofanya mazoezi na mwenza, rafiki au ndugu yako walau mara moja kwa wiki. Hii huwajengea uhusiano mzuri wa karibu tofauti na mazoea mliyozoea kuwa nayo. Mazoezi ni kiunganishi cha aina mpya ya mahusiano kati yenu.
Mazoezi pia hufukuza magonjwa. Ukitaka kupunguza uzito kwa ufanisi fanya mazoezi. Ukitaka kuwa na moyo imara fanya mazoezi. Ukitaka kuwa na figo imara fanya mazoezi kwani utatokwa na jasho na kunywa maji ya kutosha na utaondoa taka nyingi mwilini.Â
Mazoezi ni muhimu sana. Anza taratibu kwa kutembea walau dakika kumi. Hakuna ubize wowote au majukumu yanayokunyima hata dakika 20 za muda huru.Â
Tumia muda wako vizuri na tenga nafasi ya kufanya mazoezi. Utakua na mwangaza katika utendaji wako wenye kuleta tija na kufukuza magonjwa.
Dk Joshua Lameck Sultan ni daktari wa mafunzo ya mazoezi tiba katika Chuo cha Tiba na Sayansi Shirikishi Moshi (KCMC) pamoja na hospitali ya KCMC. Pia ni Mshauri katika taasisi ya Nakua na Taifa Langu (NTL) ambapo hufanya semina mbalimbali kuhusu masuala ya afya akijikita katika magonjwa yasiyoambukiza (NCD) pamoja na yale yanayoendana na mtindo maisha. Anapatikana kwa namba: +255 789 311 481, Baruapepe:Â joshualameck9@gmail.com.
Latest