Kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia kupambana na migogoro ya ardhi, ukatili Kilimanjaro

January 29, 2025 3:37 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Itatatua changamoto za kisheria mkoani Kilimanjaro kwa siku 9.
  • Dk Ndumbaro asema itatumia falsafa ya ‘gusa achia’ na ‘ubaya ubwela’.

Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amezindua kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia mkoani Kilimanjaro inayotarajiwa kupambana na matatizo ya migogoro ya ardhi na ukatili wa kijinsia yanayoripotiwa mara kwa mara mkoani humo,

Kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia ilizinduliwa Aprili 27, 2023 ikiwa na lengo la kuongeza uelewa wa sheria na upatikanaji haki katika mikoa yote nchini.

Mpaka sasa kampeni hiyo imeshafikia mikoa 17 ikiwemo mkoa wa Kilimanjaro ambapo imezinduliwa leo ikitarijawa kuendeshwa ndani ya siku tisa na kufikia halmashauri, vijiji na vitongoji vyote vya mkoa huo.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro aliyekuwa akizungumza katika uzinduzi huo ameitaja ufinyu wa ardhi sababu inayochangia tatizo la migogoro ya ardhi mkoani humo

“Waliotangulia wanasema lipo tatizo kubwa la ardhi, ni kweli kwa sababu ardhi yetu ni finyu na ilishagawanywa kwa muda mrefu kwa waliokuwa nayo na watu wanaongezeka na wanaendelea kuzaa,” amesema Babu

Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro waliojitokeza katika Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria Mkoani Kilimanjaro Leo Januari 29, 2025.

Mbali na changamoto hiyo, Babu ameitaja changamoto ya ukatili wa kijinsia kuwa miongoni mwa matatizo yanayowakabili wananchi hao licha ya kuwepo kwa madawati ya msaada wa kisheria ofisi ya mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya.

Kwa mujibu wa Babu tayari wameshawachukulia hatua za kisheria wananchi 30 waliofanya makosa ya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji na ulawiti ikiwa ni hatua ya kukabiliana na tatizo hilo mkoani humo.

Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Dk Damas Ndumbaro amesema kuwa programu hiyo ni endelevu hata baada ya siku tisa kuisha itaendelea kutolewa kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) na madawati ya msaada wa kisheria.

Amesema kuwa ndani ya siku hizo tisa na kuendelea kampeni hiyo itatatua changamoto zote zinazowakabili wananchi katika mkoa huo ikiwemo migogoro ya ardhi inayotajwa kuendelea kushamiri.

“Hakuna jiwe litaacha bila kuguswa kila mgogoro utaguswa, kushughulikiwa na kutatuliwa kila kichaka kitakatwa na kuchomwa moto,” amesema Dk Ndumbaro.

Aidha, Dk Ndumbaro amesema kuwa kampeni hiyo itaongozwa na falsafa mbili ikiwemo ya ‘gusa achia’ iliyokuwa ikitumiwa na klabu ya mpira ya miguu ya Yanga pamoja na ile ya ‘Ubaya ubwela’ inayotumiwa na klabu ya Simba.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV