JKT yatangaza nafasi za mafunzo ya kujitolea kwa vijana 2026

January 20, 2026 5:26 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Usaili utaanza rasmi Januari 26, 2026 katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani na vijana watakaoteuliwa wanatakiwa kuripoti katika kambi husika kuanzia Februari 27 hadi 4 Machi 2026.

Dar es Salaam. Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza nafasi za kujiunga na mafunzo ya kujitolea kwa mwaka 2026 kwa vijana wote wa Tanzania Bara na Visiwani, hatua inayolenga kuwajengea vijana uzalendou, ukakamavu na stadi za maisha.

Taarifa ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele iliyotolewa leo Januari 20, 2026 inabainisha kuwa vijana wanaohitajika ni wenye taaluma mbalimbali.

“Vijana wenye Vipaji vya Michezo mbalimbali, wanashauriwa kujitokeza kwa wingi kupitia Mikoa yao,” imeeleza taarifa ya Jenerali Mabele.

Mabele amesema utaratibu wa kujiungana mafunzo unaratibiwa kupitia Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambako waombaji wanaishi huku sifa kuu za waombaji zikizorodhesha katika tovuti rasmi ya jeshi hilo.

Pamoja na jeshi hilo kuwaita wenye vipaji pia liimewahimiza vijana wenye Stashahada au Shahada katika taaluma mbalimbali ikiwemo teknolojia ya habari (Tehama), sayansi ya kompyuta, uhandisi wa kompyuta, mifumo ya taarifa za biashara, usalama wa mtandao na uchunguzi wa kidijitali pamoja na mitandao ya kompyuta na uhandisi wa usalama wa taarifa kujitokeza kwa wingi. 

Usaili wa kuwapata vijana watakaojiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea utaanza rasmi Januari 26, 2026 katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani na vijana watakaoteuliwa wanatakiwa kuripoti katika kambi husika kuanzia Februari 27 hadi 4 Machi 2026.

Mafunzo hayo hayatoi ajira

Hata hivyo, JKT limeweka wazi kuwa mafunzo hayo hayatoi ajira wala halihusiki kuwatafutia ajira wahitimu wake katika taasisi, vyombo vya ulinzi na usalama au mashirika ya Serikali na yasiyo ya kiserikali. 

Badala yake, JKT hutoa mafunzo yanayolenga kuwawezesha vijana kujiajiri wenyewe baada ya kumaliza mkataba wao.

Kwa mujibu wa JKT vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo vijana hao wakati wa kuripoti vimeanishwa katika tovuti rasmi ya JKT ambayo ni www.jkt.mil.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks