Jinsi ya kukuza soko katika biashara yako

February 14, 2019 5:40 pm · Zahara
Share
Tweet
Copy Link
  • Hakikisha bidhaa yako ipo katika hali nzuri itakayowavuta wateja wako.
  • Eneo la biashara, utoaji ofa na bei vinachangia katika kukuza soko la biashara yako.

Kila mfanyabiashara au mjasiriamali ndoto yake kubwa ni kujitanua kibiashara na kuwafikia watu wengi lakini unafahamu mbinu za kukuza soko la biashara yako?

Hata hivyo sio rahisi kutoboa katika biashara kama hautakuwa mvumilivu na kufuata kanuni walizotumia wafanyabiashara waliofanikiwa duniani. 

Kama ilivyo kawaida yetu kukupa yanayokuhusu, Nukta tunakuletea njia unazoweza kuzitumia kukuza soko katika biashara yako.


Bidhaa yako ndio kitu cha kwanza

Kumbuka msingi wa biashara yako ni huduma au bidhaa unayouza. Hakikisha ina ubora na mvuto utakaomshawishi mtu kununua. Ifanye biashara yako inaongea zaidi kuliko maneno yako.

Wapo wafanyabiashara ambao wanatumia muda mwingi kutangaza bidhaa zao lakini ukweli ni kuwa haziuziki kutoka na sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwa na uhusiano wa karibu kati ya bidhaa na mteja. Hapa naamanisha bidhaa iendane na mahitaji au matakwa ya mnunuzi.

Bei ya bidhaa nayo inachangia katika ukuaji wa soko

Kumbuka lengo lolote la kufanya biashara ni kupata faida na kujitanua zaidi, lakini inategemea na bei unayowatoza wateja wako. Je bei inalingana na thamani ya bidhaa yako? 

Kumbuka, bei ya bidhaa yako inaweza kupandisha au kushusha soko lako, kuwa makini katika kuhakikisha bei ya bidhaa inaendana na hali ya mteja wako ambaye umemkusudia kumuuzia.

Kumbuka biashara yako inapaswa kuwa eneo ambalo itaonekana kwa urahisi na wateja ili uendelee kukuza soko lako. Picha|Mtandao

Boresha mazingira ya biashara yako

Hakikisha sehemu unapofanyia biashara ni safi na lenye kuvutia kuwawezesha wateja kufika na kupata huduma au bidhaa. 

Unapotafuta sehemu ya kuweka biashara lazima uwe na picha ya wateja wako kama wanaweza kufika kwa urahisi zaidi katika eneo hilo.

Sababu hiyo inawafanya wafanyabiashara wengi kuweka bidhaa kwenye  mikusanyiko ya watu kama mijini, sokoni, vituo vya magari na maeneo ambayo wateja wao wanahusika zaidi.


Zinazohusiana: Wajasiriamali wafundwa njia za kupata mitaji

                           Wanawake msisubiri kubebwa fursa za teknolojia – Wadau



Mwisho kabisa zingatia kutoa ofa

Kama umegundua kipindi cha sikukuu huwa kuna ofa nyingi za bidhaa katika maduka mbalimbali hii ni moja ya njia za kuwavutia wateja kuja kwa wingi kununua bidhaa yako.

Mathalani, kama unauza chakula unaweza  kutoa ofa ya juisi au matunda siku moja moja ili kuwavutia wateja au wengine wanaweza kutoa siku moja ya katika wiki kusema ukinunua bidhaa fulani basi utapewa kitu kingine bure.

Huduma hizo na zingine zinaimarisha ukaribu na wateja wako na kukusaidia kuongeza wigo wa soko la bidhaa.  

Enable Notifications OK No thanks