Jinsi ya kuifanya intaneti yako isionekane kwa watu

January 17, 2023 8:17 am · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Unaweza kutumia VPN na mchakato wa SSID.
  • Mbinu za ziada kuongeza uimara wa ulinzi wa mtandao wa umma.
  • Hiyo itakulinda dhidi ya wadukuzi. 

Dar es Salaam. Huenda wewe ni miongoni mwa watu ambao hawapendi intaneti (Wi-Fi) yako ionekane na watu wengine hata kama hawana nenosiri la kujiunga nayo. 

Usiwe na shaka maana unaweza kuidhibiti isionekane kwa mtu yoyote isipokuwa wewe peke yako.

Kuficha jina la intaneti hasa inayotumika na watu wengi ni njia mojawapo ya kiusalama wa kujilinda dhidi ya uvunjaji wa faragha na kupunguza uwezekano wa kudukuliwa taarifa zako.

Jinsi ya kuficha jina la mtandao wako wa Wi-Fi

Mchakato wa kuficha jina (SSID) lako la Wi-Fi ni rahisi hasa kama unatumia ‘Router’ (kigawa intaneti).  Ili kuanza, ingia kwenye paneli ya msimamizi ya router yako. Utafanya hivyo kwa kuingiza anwani yake (IP) kwenye kivinjari chako.

Ikiwa huwezi kupata anwani maalum ya router yako, wasiliana na mwongozo au tovuti ya mtengenezaji. Kulingana na kifaa chako nenda sehemu inayoitwa mpangilio ya Wi-Fi, chaguo zisizotumia waya. Tafuta chaguo la kuficha jina la mtandao wako au SSID. 

Chagua kwenye kisanduku au uzime swichi kwenye mpangilio ili kuzima kuonekana kwa jina la mtandao, kisha hifadhi mabadiliko yako. Router yako inaweza kuzima na kuwaka upya. Ili kuendelea kupata huduma, kila kifaa kilichounganishwa na mtandao awali kinapaswa kuwa na uwezo wa kuunganisha tena baada ya haya mabadiliko.


Soma zaidi: 


Kumbuka Wi-Fi hutumia masafa ya redio kusambaza taarifa kati ya kifaa chako na router. Hivyo huwezi kutegemea kuficha jina la router pekee ili kulinda mtandao wako, utaweza kumzuia jirani yako asizime au kukupotezea mtandao, lakini haitazuia mashambulizi ya mtandaoni. 

Wavamizi walio na ujuzi wa kiufundi bado wanaweza kuingilia mtandao wako hata wakati utambulisho wake umefichwa. Hii ni kwa sababu  routers huonyesha fremu ya kinara (beacon frames), ambayo hutambulisha uwepo wa mtandao.

Kwa mujibu wa Ethical Hacking Blog, fremu ya kinara ina maelezo kuhusu mtandao wako na kwa kawaida inajumuisha jina lake. Unapoficha utambulisho wako, sehemu ya jina haitajumuishwa, lakini maelezo mengine bado yatatumwa.


Njia bora za kulinda mtandao wako wa Wi-Fi

Badilisha jina la msingi la mtandao na nenosiri. Unapotumia jina la chapa ya router kutoka kwa watengenezaji humpa mdukuzi taarifa za msingi kuhusu mtandao wako na kukufanya kuwa rahisi kwa wadukuzi kujaribu kuiba taarifa zako.

Jenga desturi ya kubadilisha utambulisho wako wa mtandao na uhakikishe kuwa unachagua nenosiri thabiti na badilisha mara kwa mara. 

Tumia mtandao binafsi (VPN). VPN hufanya kazi kwenye simu kwa kuficha anwani yako ya Itifaki ya mtandao (IP) ili shughuli za kifaa chako zisiweze kufuatiliwa. VPN kwenye router chako hufanya vivyo hivyo, lakini pia italinda vifaa vingine vyote vilivyounganishwa.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW