Jinsi ya kufuta taarifa zako binafsi unapotumia programu za Google

October 11, 2022 7:35 am · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Google inakuwezesha kuondoa baadhi ya taarifa zako watu wasizione.
  • Inasaidia kujilinda dhidi ya uhalifu wa mtandaoni.

Dar es Salaam. Huenda wewe ni miongoni mwa watu ambao hawapendi baadhi ya taarifa zao binafsi zionekane wakati ukitumia huduma za kampuni ya Google ikiwemo kitafutio cha vitu mtandaoni cha Google.

Google imeweka utaratibu wa kila mtu anayetumia huduma zake kwenye simu au kompyuta kupakia taarifa zake za utambulisho ikiwemo picha, majina kamili, mwaka wa kuzaliwa. Taarifa hizo hulindwa na baadhi haziwezi kuonekana kwa umma. 

Hata hivyo, Google imeongeza uhuru zaidi ambapo watumiaji wake wanaweza kuomba kuondolewa kwa baadhi ya taarifa zao ikiwemo namba ya simu, anwani ya mahali ulipo, au ya barua pepe ili kudhibiti uwepo wako mtandaoni.

Orodha ya taarifa nyeti za binafsi ambazo Google itaondoa kwenye matokeo yake ya utafutaji inajumuisha namba za vitambulisho vya watu, namba za akaunti ya fedha, picha za vitambulisho na sahihi zilizoandikwa kwa mkono na hati za faragha kama vile rekodi za matibabu.

Unaweza pia kuitaka Google kuondoa data yoyote ya ziada ambayo inaweza kusaidia katika uwezekano wa kukutambulisha kwa wezi wa mtandaoni, kama vile maelezo binafsi ya kuingia (private login details) katika matokeo ya utafutaji.


Jinsi ya kuondoa taarifa binafsi 

Kwa kutumia kipengele cha “Results about you”, unaweza kuomba kwa urahisi kuondolewa kwa matokeo ya utafutaji ambayo yana taarifa zako binafsi ambazo hupendi zionekane mtandaoni.

Google ilitangaza katika sasisho la chapisho la blogu mwishoni mwa Septemba 2022 kwamba sasa inasambaza kipengele hicho kwa watumiaji wa simu za mkononi, ingawa haijulikani ni kwa haraka kiasi gani usambazaji huu unafanyika.

Sasa ukiwa mtandaoni hutakuawa na wasiwasi kwa taarifa zako kuonekana kwa watu wengine kwa sababu unaweza kuzidhibiti. Picha| David Matambo.

Fata hatua zifuatazo kukamilisha zoezi hili:

  1. Fungua programu ya simu ya mkononi ya Google.
  2. Gusa aikoni ya wasifu wako kwenye kona ya juu kulia ya programu.
  3. Tafuta “Matokeo kukuhusu” kwenye menyu inayofunguka.
  4. Gusa vidokezo vinavyowasilishwa ndani ya zana ili kuipa Google maelezo inayohitaji ili kutathmini na ikiwezekana kuondoa matokeo ya utafutaji yaliyo na data yako ya faragha.

Unaweza pia kutuma maombi ya kuondoa matokeo mahususi ya Tafuta na Google ambayo yana maelezo nyeti na binafsi yanapoonekana unapotafuta mambo yanayokuhusu  kwa kugusa ikoni ya nukta tatu karibu na matokeo ya Tafuta na Google.

Utafuata ukurasa wa “Kuhusu matokeo haya” unaohusiana na chanzo. Ikiwa akaunti yako ya Google tayari ina idhini ya kufikia zana mpya ya ombi la kuondolewa, unapaswa kuona chaguo la “Ondoa matokeo” chini ya ukurasa.

Unaweza pia kuondoa maelezo yako binafsi bila ya kulazimika kutumia programu ya tafuta na Google kupitia mtandao moja kwa moja.


Soma zaidi:


Ili kufanya hivyo, utahitaji kutembelea kitatuzi kinachopatikana kwenye tovuti ya Usaidizi wa Google, kisha ufuate hatua zilizo hapa chini:

  1. Teua chaguo la “Ondoa maelezo unayoona kwenye Utafutaji wa Google”.
  2. Ndani ya sehemu yenye kichwa “Maelezo ninayotaka kuondolewa ni,” chagua “Katika matokeo ya utafutaji wa Google na kwenye tovuti.”
  3. Unapoulizwa ikiwa umewasiliana na mmiliki wa tovuti, chagua “Hapana, sipendi kufanya hivyo.”
  4. Chagua aina ya maelezo binafsi ambayo ungependa yaondolewe kwenye matokeo ya Utafutaji wa Google.
  5. Ingiza maelezo yaliyoombwa, ikijumuisha viungo vya kurasa zilizo na maudhui unayotaka kuondolewa.

Kuambatisha picha ya skrini ya ukurasa (Screenshot) wa wavuti ambayo ina maelezo binafsi inapendekezwa ili kuharakisha mchakato wa ombi la kuondolewa, lakini si lazima. Unaweza pia kutoa maelezo ya kina zaidi ya muktadha ikiwa unataka.

Baada ya Google kuidhinisha ombi la kuondoa maelezo yako binafsi, itaacha kujumuisha tovuti zilizo na data zikuhusuzo katika matokeo yake yote ya utafutaji au hasa katika utafutaji unaojumuisha jina lako. Ikiwa ombi lako halijaidhinishwa, hakuna mabadiliko yatafanywa.

Hata hivyo, Google haiwezi kuondoa moja kwa moja maudhui yanayoonekana kwenye tovuti au. Pia baadhi ya watu bado wanaweza kupata maelezo yako kwenye tovuti hiyo ikiwa watatumia injini tofauti ya utafutaji kama vile Bing na DuckDuckGo.

Ikiwa ombi lako la kuondolewa limekataliwa na Google au ukitaka maudhui yaondolewe kwenye tovuti basi utahitaji kuwasiliana moja kwa moja na mmiliki wa tovuti na kumwomba aondoe maudhui yanayohusiana na wewe.

Msimamizi wa tovuti akikubali ombi lako na kuondoa taarifa zako binafsi, hazitapatikana tena kwa watumiaji hata kama watatafuta kwa kutumia injini ya utafutaji tofauti na Google.

Kuanzia mapema mwaka ujao, utaweza kuchagua kupokea arifa (alert) ikiwa matokeo mapya yenye maelezo yako ya mawasiliano yatatokea, ili uweze kuomba ziondolewe haraka.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.