Jeshi la ukoaji Mwanza laainisha maeneo hatarishi kuelekea mvua za El-Nino

October 19, 2023 3:46 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na baadhi ya maeneo katika wilaya za Nyamagana, Ilemela, Magu na misungwi.
  •  Visiwa zaidi ya 60 kikiwemo kisiwa cha Juma na  Chabagadi vyatajwa.
  • Jeshi la zimamoto na ukoaji laanza mazoezi na kuongeza vifaa.

Mwanza. Siku chache baada ya Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) kutoa taarifa ya uwepo wa mvua kubwa za El-Nino, jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Mwanza limewataka wakazi wanaoishi kwenye maeneo hatarishi kuanza kuchukua tahadhari ya kuhamia kwenye maeneo ya miinuko.

Miongoni mwa maeneo yanayotajwa kuwa hatarishi ambayo hukusanya maji mengi kutoka kwenye mitaro mbalimbali wilayani Nyamagana ni pamoja na mtaa wa Mabatini, daraja la Maasai, mto Mirongo, Mkuyuni na Nyashishi darajani.

Mengine ni yale yaliyopo wilayani Ilemela ambayo ni Kilimahewa, Kirumba na Nyamhongolo, wilayani Misungwi (maeneo ya Mwagiligili, Mwasonge na Ngaya) pamoja na maeneo ya Kisamba na Ngashe yaliyopo wilayani Magu.

Pia Jeshi hilo limeanisha visiwa zaidi ya 60 kikiwemo kisiwa cha Juma na  Chabagadi vilivyopo wilayani Ukerewe na vingine vilivyopo Sengerema kuwa miongoni mwa maeneo hatarishi katika kipindi cha mvua za El-Nino.

Akizungumza na Nukta habari, Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Mwanza, Camila Laban amewataka wananchi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari wakati wote zitakaponyesha mvua hizo.

“Tunaomba wananchi pale watakapoona kuna maji mengi kwenye maeneo hayo wasijaribu kuyavuka na sisi kama jeshi la zimamoto kwenye madaraja hayo mvua zitakapoonekana kubwa tutapeleka askari kwa ajili ya kufunga njia ili wananchi waweze kuchukua tahahadhari,” amesema Laban.  


Soma zaidi:Tanzania yachaguliwa makamu wa rais mkutano wa 25 wa UNWTO


Itakumbukwa kuwa Oktoba 8 mwaka huu TMA ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu uwepo wa mvua za kubwa kuanzia mwezi Oktoba hadi Disemba zinazoweza kusababisha matukio ya vifo, magonjwa ya mlipuko na uharibifu wa miundombinu.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Ladislaus Chang’a, mvua hizo za vuli zitakuwa za wastani na wastani wa juu ambapo zitanyesha katika pwani ya kaskazini na ukanda wa Ziwa Victoria.

Licha ya kutoa tahadhari hizo, Laban amesema jeshi la uokoaji limeanza kufanya mazoezi pamoja na kuongeza vifaa vya kukabiliana na mvua hizo ili kunusuru wananchi.

“Pamoja na mazoezi pia, tunaishauri jamii hususani wanaokaa kwenye mabonde kuhamia kwenye miinuko, wananchi watoe taarifa kwenye kamati za maafa au kupiga simu ya dharura,” amesema Laban

Aidha, kiongozi huyo amewataka wazazi kutoa elimu kwa watoto wa shule za msingi kuwasindikiza kwenda shule katika kipindi chote cha mvua ili kuhakikisha wanafika salama shuleni.

Wananchi wataka utunzaji wa mazingira

Judith Ferdinand ni mkazi wa Nyamanoro Mashariki mkoani Mwanza, amewataka wakazi wenye tabia za kutupa takataka kwenye mitaro kuacha mara moja kwani zinachangia mafuriko na maji kuingia katika makazi yao.

“zipo tabia za baadhi ya wananchi kutupa taka kwenye mitaro ambazo zinachangia kuziba mifereji inayopitisha maji, tabia hizo waziache…

…Ikiwezekana mamlaka zinazohusika na masuala ya mazingira ziaze kutoa elimu na kuzibua mitaro ili kuondoa adha inayoweza kujitokeza,” amesema Judith.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA AKIHITIMISHA MAFUNZO YA UONGOZI NGAZI YA JUU, UONGOZI DARAJA LA PILI KOZI 2025/26

🔴LIVE: RAIS SAMIA AKIHITIMISHA MAFUNZO YA UONGOZI NGAZI YA JUU, UONGOZI DARAJA LA PILI KOZI 2025/26

Nukta TV

Rais Samia: Anzisheni mfuko  kuwasaidia wafungwa wenye ujuzi wanapotoka gerezani

Rais Samia: Anzisheni mfuko kuwasaidia wafungwa wenye ujuzi wanapotoka gerezani

Nukta TV

🔴LIVE: RAIS SAMIA AKIHITIMISHA MAFUNZO YA UONGOZI NGAZI YA JUU, UONGOZI DARAJA LA PILI KOZI 2025/26

🔴LIVE: RAIS SAMIA AKIHITIMISHA MAFUNZO YA UONGOZI NGAZI YA JUU, UONGOZI DARAJA LA PILI KOZI 2025/26

Nukta TV