Jakarta inapozama baharini, Indonesia inajenga mji mkuu mpya

August 28, 2019 7:26 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ujenzi wa mji huo unatarajiwa kuanza mapema mwaka 2021 na kukamilika mwaka 2024.
  • Mji huo utachukua nafasi ya uliopo sasa wa Jakarta ambao umeanza kuzama. 
  • Mji huo umekuwa ukikumbwa na mafuriko mara kwa mara kwa sababu uko karibu na fukwe za bahari. 

Katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo kuongezeka kwa kina cha bahari, nchi ya Indonesia iko katika mpango wa kujenga mji mkuu mpya ili kuchukua nafasi ya uliopo sasa wa Jakarta ambao umeanza kuzama. 

 Mji Mkuu wa Jakarta wenye wakazi zaidi ya milioni 10 uko pwani ya Kaskazini Mashariki mwa kisiwa cha Java kilichozungukwa na bahari ya Hindi na Java. 

Agosti 26, 2019, Rais wa nchi hiyo, Joko Widodo alitangaza mpango huo wa kujenga mji mpya wenye kila kitu ikiwa ni hatua ya kukabiliana na athari za kuzama kwa Jiji la Jakarta siku zijazo. 

Ujenzi wa mji huo unatarajiwa kuanza mapema mwaka 2021 na kukamilika mwaka 2024, wakati Widodo akikamilisha kipindi cha pili cha uongozi wake. 

 “Kama nchi kubwa iliyopata uhuru miaka 74 iliyopita, Indonesia haijawahi kuchagua mji wake mkuu,” amenukuliwa Rais Widodo na shirika la habari la AFP na kuongeza kuwa, “Mzigo wa Jakarta tulionao ni mkubwa sana kwa sababu ni kituo cha Serikali, biashara, shughuli za fedha na huduma.”

Mji mkuu mpya unaotarajiwa kujengwa uko katikati ya kisiwa cha Borneo, karibu kabisa na jiji la Balikpapan na Samarinda.

Serikali ya Indonesia imesema imefanya utafiti wa kina kwa miaka mitatu iliyopita na matokeo yake yanaonyesha kuwa eneo linalofaa kwa ujenzi huo ni  sehemu ya kaskazini ya ukanda wa Penajam Paser  na sehemu ya Kutai Kartanegara huko Mashariki mwa mji wa Kalimantan. 


Soma zaidi:


Kuhusu gharama za kuhamisha mji huo, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa itagharimu Dola za Marekani bilioni 34 (Sh78.2  trilioni) ambapo asilimia 19 ya fedha hizo zitatoka serikalini na kiasi kilichobaki kitatoka kwa wawekezaji binafsi.

Kuzama kwa Jakarta inaweza isiwe jambo la kushangaza kwa sababu eneo lake lina chemichemi nyingi halafu liko karibu na bahari na kuliweka katika hatari ya kukumbwa na mafuriko mara kwa mara. 

Indonesia ni miongoni mwa maeneo mengi yaliyoathiriwa na kuongezeka kwa kina cha bahari, jambo linalotishia maisha ya watu na miundombinu ya miji iliyopo karibu na bahari. 

Mipango hiyo ya Indinesia pia inatoa somo kwa miji mingine ikiwemo Dar es Salaam kuchukua hatua kabla maeneo yao hayajazama kabisa siku zijazo. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Msemaji Geita: Vijana msikurupuke kuja Katoro

Msemaji Geita: Vijana msikurupuke kuja Katoro

Nukta TV

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV