Haya ndio maajabu ya iPhone Duo simu mpya kutoka Apple
- Oda za awali za mauzo kuanza Oktoba 16, huku mauzo rasmi yakitarajiwa kuanza Oktoba 23, 2026.
- Maajabu ya hii simu yapo kwenye kioo chake ambacho kina ukubwa wa inchi 5.4 ikiwa haijakunjuliwa na ukubwa wa inchi 7.6 ikiwa imekunjuliwa.
Dar es Salaam. Kila kona ya mitandao ya kijamii kwa sasa stori kubwa inayobamba ni kuhusu iPhone baada ya kampuni ya Apple kuzindua toleo jipya la Iphone 18 na iPhone Duo.
Hata hivyo, mjadala mkubwa kwa mwaka huu haupo kwenye ‘series’ ya Iphone 18, bali kwenye iPhone Duo simu yenye kioo kinachokunjika iliyoingizwa kwa mara kwanza sokoni na kampuni hiyo.
Maajabu ya hii simu yapo kwenye kioo chake ambacho kina ukubwa wa inchi 5.4 ikiwa haijakunjuliwa na ukubwa wa inchi 7.6 ikiwa imekunjuliwa.
Kwa wale wapenzi wa kutazama movies, ‘animations’ au kucheza gemu hapa nafikiri Apple itakuwa imewakonga moyo.
Kwa upande wa chaji, iPhone duo inauwezo wa kuchaji ‘wireless’ yaani kuchaji bila kuchomeka waya, na ikiwa imejaa full, chaji yake inauwezo wa kudumu kwa saa 44 takriban siku 2 ikiwa utatumia skrini ndogo na ikiwa utatumia skrini kubwa chaji yake inaweza kudumu hadi saa 31 sawa siku moja na masaa saba.
Lakini pamoja na kukaa chaji kwa muda wote huu iPhone Duo inaweza kuingiza chaji kwa asilimia 50 ndani ya dakika 20 tu.
Kwa upande wa kamera, simu hii ina kamera mbili za nyuma ambapo kamera kuu inauwezo wa megapixel 48, na kamera ya mbele ikiwa na uwezo wa megapixel 12.
Tofauti na matoleo mengi mapya ya iPhone ulinzi wa iPhone Duo haujahusisha uwezo wa kufungua simu hii kwa kutumia FaceID na badala yake utaweza kufungua kwa fingerprint kupitia touch ID iliyowekwa pembeni ya kitufe cha kuwashia.
Kama ambavyo simu hii ni kali basi na bei yake pia imechangamka kidogo kwa sababu Apple imeweka bei ya kuanzia ya iPhone Duo kuwa Dola za Marekani 1,999, sawa na takribani Sh5.3 milioni ikiwa ni nje ya gharama za usafirishaji pamoja na kodi.
Kwahiyo mpaka simu hiyo inakufikia hapa bongo unaweza kuipata kwa gharama ya hadi Sh7 milioni au zaidi kutegemea na duka utakaloenda kununua.
Kwa bei hiyo, Duo inakuwa miongoni mwa simu zinazozalishwa na kampuni ya Apple zenye gharama kubwa zaidi, huku bei yake ikiwa juu ikilinganishwa na iPhone 18 Pro ambayo Apple waliizundua pia katika uzinduzi ulifanyika Septemba 9, 2026.
Hata hivyo, kelele zimekuwa nyingi sana kutoka kwa mtani wa jadi na mshindani mkubwa wa kibiashara wa iPhone ambaye ni Samsung ambapo wengi wamedisi teknolojia hiyo wakisema kwamba hakuna kitu kipya kwani ilishatumika na kampuni nyingine kama vile Samsung na Huawei miaka mingi iliyopita.
Samsung ambaye ndiye mtengenezaji mkubwa wa vioo pamoja na kamera za simu za iPhone, ndiyo kampuni ya kwanza kutumia teknolojia ya vioo halisi vinavyokunjika miaka 6 iliyopita kupitia toleo lake la Galaxy Z Flip.
Apple imepanga kuanza kupokea oda za mauzo ya iPhone Duo kuanzia Oktoba 16, huku mauzo rasmi yakitarajiwa kuanza Oktoba 23, 2026.
Vipi, na wewe uko tayari kununua simu hiyo kwa zaidi ya milioni 5 au tukuache kwanza?
2 thoughts on “Haya ndio maajabu ya iPhone Duo simu mpya kutoka Apple”
Comments are closed.
Makala hii inaonyesha jinsi kamera na skrini vinavyoendelea kuwa sehemu muhimu ya uzoefu wa simu. Kwa mtumiaji anayepiga picha za bidhaa, safari au matukio ya kila siku, uwezo wa kuboresha picha bila kupoteza mwonekano wa asili ni muhimu kama ubora wa kamera yenyewe. Zana za AI zinaweza kusaidia kuondoa vitu visivyohitajika, kubadili mandhari, kusawazisha mwanga na kujaribu mtindo mpya huku picha ya awali ikibaki salama.
Kwa anayeanza kujifunza uhariri wa picha, ni vizuri kuanza na nakala ya picha, kuandika maelekezo mafupi na kulinganisha matokeo na picha halisi kabla ya kushiriki. Pia hakikisha una ruhusa ya kutumia picha za watu wengine na usitumie uhariri kuwapotosha watazamaji. Rasilimali ya kujaribu uhariri wa picha kwa picha ni image to image ai, ambayo inaweza kusaidia kuelewa tofauti kati ya kubadili mtindo na kubadili maudhui ya picha. Hii ni nyongeza nzuri kwa mjadala wa teknolojia ya simu unaoelezwa hapa.
Nyongeza nzuri kwenye mjadala huu ni namna teknolojia ya simu inavyoweza kuwasaidia watayarishaji wa maudhui wa Tanzania. Kabla ya kuchapisha picha, ni busara kuhifadhi faili la awali, kutumia mwanga wa kawaida kama rejea na kuangalia kama rangi za ngozi, maandishi na nembo zimebaki sahihi baada ya uhariri. Kwa picha za biashara, uaminifu ni muhimu: mabadiliko ya kisanii yawekwe wazi na picha za watu zitumike kwa ridhaa yao. Wanaojifunza wanaweza kuanza kwa kujaribu zana ya image to image ai hapa: https://imgtoimg-ai.com/ na kulinganisha matokeo katika ukubwa wa simu na kompyuta. Hatua hizi ndogo husaidia kupata picha safi bila kupotosha hadhira.