Google, Meta kutambulisha bidhaa mpya Oktoba

September 7, 2022 8:42 am · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni simu, saa, vifaa vya kusikilizia muziki na uhalisi pepe.
  • Vifaa hivyo vinatarajia kuongeza ushindani katika soko la mawasiliano duniani.          

Dar es Salaam. Kampuni kubwa za teknolojia za Google na Meta za nchini Marekani zinatarajia kutambulisha bidhaa zao mpya zikiwemo simu mwezi ujao wa Oktoba, ikiwa ni hatua kuwasogea wateja wao ladha mpya ya vifaa vya kielektroniki.

Google katika ukurasa wake wa Twitter imethibitisha kuwa itaandaa hafla ya “Made By Google” mnamo Oktoba 6, 2022 ambapo kampuni hiyo itatumbulisha simu mpya aina ya Pixel 7, Pixel 7 Pro na saa janja za Google Pixel.

“Yote yanakuja pamoja. Jiunge nasi moja kwa moja kwa #MadeByGoogle mnamo Oktoba 6,” umeleeza ujumbe wa Google katika mtandao wa Twitter. 

Google imesema simu ya Pixel 7 itatumia mfumo endeshi wa Android 13 na itaangazia kizazi kijacho cha chipu maalum ya kampuni hiyo (Tensor) ili kuihamisha kampuni kutoka kwa vichakataji vya “Qualcomm.”

Saa janja ya Pixel ndiyo saa mahiri ya kwanza iliyoundwa na Google, imeundwa kufanya kazi na simu zingine zote za Pixel na Android, pamoja na vifaa vya masikioni visivyotumia waya vya Pixel.

Kwa mujibu wa kamouni hiyo, baada ya kutambulishwa kwa bidhaa hizo Oktoba 6, zitaanza kuuzwa siku hiyo hiyo.


Soma zaidi:


Baada ya Google wanafuata Meta

Ni bandika bandua, Google wakitambulisha bidhaa zake, Meta, kampuni mama ya mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram, Messenger na WhatsApp nayo inatarajia kuingiza sokoni bidhaa mpya ya uhalisia pepe (Virtual Reality). 

Tukio la kuitambulisha bidhaa hiyo litafanyika Oktoba 11 wakati mkutano wa Meta utakaofanyika Marekani, siku sawa na iliyotumika kubadilisha jina la kampuni kutoka Facebook hadi Meta. 

“Mwaka jana, tulishiriki maono yetu ya Metaverse. Jifunze kuhusu tulipo leo, na nini kitakachofuata. Jiunge nasi mnamo Oktoba 11 kwa Meta Connect,” kiimechapisha chumba cha habari cha Meta kupitia ukurasa wa Twitter.

Siku hiyo, Meta itatoa maelezo kuhusu kifaa chake cha uhalisia pepe kijacho, ambacho kampuni imekuwa ikikinadi kwa muda sasa  chini ya jina la msimbo “Project Cambria”.

Uhalisia pepe itakuwa nyepesi, nyembamba na yenye starehe zaidi kuliko zilizopo sasa za “Quest 2”. Meta inalenga zaidi matumizi ya uhalisia pepe, hivyo kuruhusu watumiaji kujumuisha mazingira yao ya ulimwengu halisi katika programu hizo. 

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.