Gigachat: Mshindani mpya wa ChatGPT

April 26, 2023 9:47 am · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Inatarajiwa kuleta mapinduzi katika sekta ya benki.
  • Imetengenezwa Urusi kwa kushirikiana na kampuni ya Microsoft. 

Dar es Salaam. Benki kubwa zaidi ya Urusi, Sberbank mwanzo wa wiki hii imetangaza kuzindua programu tumishi ya GigaChat, chatbot inayoendeshwa na teknolojia ya akili bandia (AI) iliyoundwa kuleta mapinduzi ya huduma kwa wateja katika sekta ya benki. 

Programu hiyo imeundwa kwa kushirikiana na kampuni ya Microsoft OpenAI na kufunzwa mahususi kwa lugha ya Kirusi.

GigaChat hutumia modeli ya lugha ya GPT-3 kutoa huduma binafsi za kibenki kwa ufanisi. Kwa sasa, inapatikana tu katika hali ya majaribio ya mwaliko pekee.

Hatua hii inatarajiwa kurahisisha shughuli mbalimbali kwa wateja wa benki, ikiwa ni pamoja na kuangalia salio la akaunti, kuhamisha fedha, kulipa bili, na kupanga miadi na wawakilishi wa benki.

Benki Kuu ya Urusi imefanya uwekezaji huu mkubwa katika teknolojia ikiwa ni juhudi za kupunguza utegemezi wa nchi hiyo katika utoaji wa huduma za kifedha na uagizaji wa bidhaa duniani.

Imeelezwa kuwa GigaChat ni moja ya “matunda” ya uwekezaji wake katika uwanda wa  teknolojia ili kuvuka vikwazo vikali vya chi za Magharibi dhidi ya shughuli za Moscow nchini Ukraine.

Hatua hii ya Sberbank ni dalili ya wazi ya kuongezeka kwa umuhimu wa teknolojia ya AI katika ulimwengu wa biashara na uwezekano wake wa kubadilisha viwanda na kuboresha maisha ya watu duniani kote. 

ChatGPT ni akili bandia/AI ambayo imejifunza mifano mingi ya taarifa/data ya maneno, hii imeifanya iweze kuelewa swali na kutoa majibu yenye asili kama ya binadamu.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Fahamu kuhusu 'BIPOLAR' | Ugonjwa hatari unaoathiri na kubadili hisia

Fahamu kuhusu 'BIPOLAR' | Ugonjwa hatari unaoathiri na kubadili hisia

Nukta TV

Je, ’BIPOLAR’ ina uhusiano na kupenda kufanya tendo la ndoa zaidi?

Je, ’BIPOLAR’ ina uhusiano na kupenda kufanya tendo la ndoa zaidi?

Nukta TV

Hii ndio sababu uhusiano wa kimapenzi ni marufuku makazini

Hii ndio sababu uhusiano wa kimapenzi ni marufuku makazini

Nukta TV