Gharama za uagizaji chakula kuongezeka kwa asilimia 10 duniani
- Zinakadiriwa kuwa zitapanda hadi Dola za Marekani trilioni 1.94.
- Hiyo itasababishwa na kupanda kwa bei za vyakula.
Dar es Salaam. Wakati mfumuko wa bei ukipanda hadi kufikia asilimia 4.9 kwa mwaka unaoishia Oktoba 2022 nchini Tanzania, gharama ya kimataifa ya uagizaji chakula kutoka nje inakadiriwa kupanda hadi Dola za Marekani trilioni 1.94 mwaka huu 2022 zaidi ya ilivyotarajiwa hapo awali.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), mfumuko huo wa bei umeongezeka kutoka asilimia 4.8 iliyorekodiwa mwaka unaoishi Septemba 2022 ambao umechangiwa na kuongezeka kwa bei za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula ikiwemo mchele.
Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) inaeleza kuwa utabiri huo mpya ulioainishwa katika mtazamo wa chakula wa FAO umedhihirisha kiwango cha juu zaidi na ongezeko la asilimia 10 zaidi ya kiwango kilichoweka rekodi cha mwaka 2021.
Hata hivyo, kasi ya ongezeko hilo inatarajiwa kupungua kutokana na ongezeko la bei ya juu ya chakula duniani na kushuka kwa thamani ya sarafu dhidi ya dola ya Marekani.
Sababu zote hizo mbili zinapima uwezo wa kununua wa nchi zinazoagiza chakula na, baadaye, kiwango cha chakula kinachoagizwa kutoka nje.
Sehemu kubwa ya ongezeko la gharama hizo linachangiwa na nchi zenye mapato ya juu, kutokana na bei ya juu zaidi duniani, huku viwango hivyo pia vikitarajiwa kupanda.
Ripoti hiyo inayohusu masuala ya chakula inaeleza kuwa makundi ya nchi zilizo katika mazingira magumu kiuchumi yanaathiriwa zaidi na bei ya juu.
Mathalan, gharama za jumla za uagizaji wa chakula kwa kundi la nchi za kipato cha chini unatarajiwa kubaki bila kubadilika ingawa unatabiriwa kupungua kwa asilimia 10 katika kiwango cha uagizaji, ikiashiria kuongezeka kwa ufikiaji wa chakula hicho kwa nchi hizo.
“Hizi ni dalili za kutisha kulingana na mtazamo wa uhakika wa chakula, zinaonyesha waagizaji wanapata ugumu wa kufadhili kupanda kwa gharama za kimataifa, na hivyo kuashiria mwisho wa kustahimili bei ya juu ya kimataifa,” imeonya ripoti hiyo kutoka kitengo cha masoko na biashara cha FAO.
Pengo lililopo kuongeza athari
Ripoti hiyo ya mtazamo wa chakula, ambayo inaainisha mifumo ya biashara ya chakula na makundi ya chakula, inaonya kuwa tofauti zilizopo zinaweza kuwa mbaya zaidi, huku nchi zenye mapato ya juu zikiendelea kuagiza bidhaa za chakula kutoka kwa wigo mzima wa bidhaa za chakula, wakati kanda zinazoendelea zikizingatia vyakula vikuu pekee.
FAO inakaribisha idhini ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) ya upenyo wa mshtuko wa Chakula kwa msingi wa pendekezo la FAO la usaidizi wa ufadhili wa uagizaji wa chakula kama hatua muhimu ya kupunguza mzigo wa kuongezeka kwa gharama za uagizaji wa chakula miongoni mwa nchi za kipato cha chini.
“Athari mbaya kwa pato la kilimo duniani na uhakika wa chakula huenda zikaendelea hadi mwaka 2023,” imeeleza FAO.
Latest
