Fisi aua mtoto wa miaka 9 Mwanza

March 18, 2024 12:44 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Wanafamilia waeleza jinsi tukio lilivyotokea.
  • Wakazi wa kijiji cha Nyamahona waitaka Serikali kuchukua hatua kumdibiti mnyama huyo.

Mwanza. Pendo Kulwa(9) mkazi wa Kijiji cha Nyamahona wilayani Sengerema mkoani Mwanza amefariki dunia baada ya kushambuliwa na fisi wakati alipoenda kuchanja kuni akiwa na wenzake.

Babu wa marehemu Theonest Ncheye, ameiambia Nukta Habari jinsi alivyopata taarifa za kifo cha mjukuu wake aliyepoteza maisha (jana) Machi 17, 2024 ambapo alienda kukata kuni mlimani kama ilivyo kawaida yake na  watoto wengine wa kijiji hicho.

“Tulisikia kipenga kikitutaarifu kwenda kutafuta mwili wa mtoto ambaye ameshambuliwa na fisi mlimani na tulipoenda kuanza kumtafuta nilikuta ni mjukuu wangu,fisi ameshamuua na baadhi ya sehemu amemla,”amesema Ncheye

Naye Suzana Mashimba, Bibi wa marehemu huyo ameelezea masikitiko yake baada ya kumpoteza mjukuu wake na kuiomba Serikali kuhakikisha wanamtafuta mnyama huyo na kumuua ili asiendelee kuleta madhara kwa watu wengine.


Soma zaidi:Tanzania yajipanga kukabiliana maafa ya mionzi na kemikali


Fisi ni tatizo kwa wakazi wa Nyamahona

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyamahona, Paulo Shingashinga amesema hilo ni tukio la tatu kutokea ndani ya muda mfupi ambapo fisi huyo ameua mwanafunzi mmoja na wengine wawili kujeruhiwa ambao wamelazwa katika hospitali ya misheni iliyopo Sengerema.

“Tuliutaarifu uongozi wa kata pamoja na maafisa wanyamapori ili wasaidie katika kudhibiti wanyama hao ambao wanazua taharuki hususani wanafunzi wanapoenda shule asubuhi,” amesema Shingashinga

Aidha, juhudi nyingine zinazotarajia kufanyika kumdhibiti mnyamahuyo i pamoja na  kutafuta kikundi maarufu cha kuua Wanyama hao kilichopo Misungwi.

Kwa upande wake mtendaji wa kata hiyo, John Bupamba amewataka wananchi kuchukua tahadari wakati juhudi mbalimbali za kutafuta wanyama hao kwenye milima zikiendelea.

Wakati huo huo, wananchi katika kjiji hicho wameiomba Serikali kutafuta suluhu ili kunusuru wananchi kuendelee kuuliwa na wanayama hao.

“Ni tukio la kushangaza ambapo zamani tulizoea Wanyama hao walikuwa wanashambulia fisi au kondoo, hatukuwahi kusikia wakidhuru binadamu, zinahitajika juhudi za kimakusudi ili kuhakikisha Wanyama hao wanauawa ili wasiendelee kudhuru binadamu,” amesema Filipo Gabriel mkazi wa Nyamagona.

1 thought on “Fisi aua mtoto wa miaka 9 Mwanza

Comments are closed.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV