Farasi wanavyotumika katika ulinzi, kukuza utalii katika miji mikubwa
- Wanatumika kutuliza ghasia na kutawanya makundi ya watu ambao hawawezi kudhibitiwa na askari polisi wanaotumia magari
- Ni alama ya utamaduni na kivutio cha kwa wageni wanaotembelea miji mikubwa duniani.Â
- Ni hodari katika katika uokozi na kuyafikia maeneo yasiyofika na magari.Â
Huenda wewe ni miongoni mwa watu ambao wamewahi kutembelea miji mikubwa duniani na umeshuhudia farasi wanaoongozwa na askari waliovalia sare wakizunguka katika mitaa mbalimbali lakini hufahamu sababu za wanyama hao kuwepo mjini?
Farasi ambao ni warefu wa kimo hutumika zaidi kwa shughuli za usalama wa raia na mali zao. Lakini kwanini farasi na siyo teknolojia nyingine za usalama kama matumizi ya taa na kamera maalum za CCTV au vizuizi vya barabarani?
Hizi ndizo sababu, miji mbalimbali duniani kuwa na kikosi maalumu cha farasi (Mounted police) wanaoongozwa na askari polisi:Â
Kudhibiti fujo na vurugu za watu
Sababu kubwa ya farasi unaowaona katika majiji makubwa ikiwemo London nchini Uingereza, New York (Marekani) na Berlin (Ujerumani) ni kutuliza ghasia wakati makundi mbalimbali ya watu yakizozana.Â
Polisi wanaotumia farasi hao wana uwezo mkubwa wa kuvunja na kutawanya mkusanyiko wenye fujo, hasa kwenye mechi za mpira wa miguu. Â Â
Farasi zinaweza kupenya kwa urahisi katikati ya umati wa watu na ni rahisi kwa polisi aliye juu ya mnyama huyo kuwaona watu na kujihami kwa lolote wakati akitekeleza majukumu yake.
Pia mnyama huyo anaweza kukimbia kwa haraka na kupenya kwenye maeneo yaliyobanana kama mitaa yenye maduka na pembezoni mwa barabara.
Askari anayetumia farasi anaweza kudhibiti fujo kwa muda mfupi kuliko anayetumia gari. Picha|Mtandao.
Ukubwa wa mnyama huyo
Sababu ya askari wanaoutumia farasi kuwa na ufanisi mkubwa hasa kudhibiti na kutawanya umati wa watu ni kwa sababu farasi ni mnyama mkubwa ambaye wanasaikolojia wanadai kuwa humjengea hofu binadamu ambayo inahusishwa na watu kuogopa wanyama hao ambao wanaweza kuwadhuru.
Kama kuna fujo, watu hawatafikiri mara mbili kabla ya kuharibu au kuchoma gari la polisi, lakini ni tofauti kabisa kwa mnyama mkubwa ambaye na yeye anajihami wakati wa kupambana naye.Â
Zinazohusiana:Â
- Tanzania yaangazia masoko 18 duniani kukuza utalii
- Tanzania yang’ara tena tuzo za eneo bora la utalii duniani
Ni heshima na ufahari
Farasi anahusishwa katika  historia, tamaduni na desturi za nchi mbalimbali duniani.Â
Katika nchi za Sweden na Scotland, askari anayepanda farasi siyo tu anatumikia jeshi la polisi, lakini anawakilisha utambulisho wa jinsi farasi anavyotimiza majukumu yake kikamilifu ambayo hayawezi kufanywa na mtu mwingine.Â
Kwao ni heshima na ufahari, kwa myama huyo mwenye umbo kubwa kuzunguka katika mitaa.
Â
 Urafiki na kuvutia
Watu wengi wanafikiri askari wanaopanda farasi kwa kiasi fulani wanawachukulia kama marafiki kwa sababu wanafikika na kuvutia kuliko polisi ambao wako kwenye magari yaliyo na vioo vikubwa.Â
Watu wengi wanaweza kumsogelea askari aliyepanda farasi kuliko yule aliyepo kwenye gari. Farasi wananogesha urafiki kati ya raia na polisi.Â
Lakini wanyama hao wanatumika kama kivutio kwa wageni wanaotembelea miji mbalimbali duniani. Ni fursa ya kukuza utalii katika miji mikubwa.Â
Farasi siyo tu ni kivutio bali ni kiunganishi muhimu kati ya raia na askari polisi. Picha|Mtandao.
Farasi ni hodari katika shughuli za uokozi
 Askari wanaopanda farasi wanafundishwa pia kusimamia shughuli za utafutaji na uokoaji hasa katika kipindi cha majanga kama mafuriko. Wana uwezo wa kubeba vifaa vingi vya uokozi na kuyafikia maeneo hatarishi ambayo hayafikiki na magari.  Â
Katika eneo lako, farasi wanatumika kwa shughuli zipi?