Facebook App yaja kivingine

April 9, 2019 3:12 pm · Daniel
Share
Tweet
Copy Link


Muonekano wa ukurasa wa Facebook App ambao unatoa sababu za kwanini mtumiaji anapokea matangazo kwenye ukurasa wake.Picha|Mtandao.


  • Sasa kuwawezesha watumiaji wake kufahamu kwanini matangaza ya biashara au habari zinawafikia katika kurasa zao.
  • Hayo ni miongoni mwa maboresho yanayofanywa na Facebook ili kuwarahisishia watumiaji wake upatikanaji wa huduma bora zinazokidhi mahitaji yao.

Dar es Salaam. Katika kuhakikisha inasogeza huduma zake karibu na watumiaji, mtandao wa Facebook umefanya maboresho katika programu yake tumishi (Facebook App) ambapo mtumiaji ataweza kupata sababu zinazoeleza kwanini tangazo au habari imewekwa kwenye ukurasa wake. 

Hatua hiyo huenda ikatatua changamoto ya watumiaji wa mtandao huo kupata matangazo bila ridhaa yao au bila kujua sababu za tangazo husika kuwekwa kwenye ukurasa.

Maboresho hayo yanajikita katika mambo mawili ya “Kwa nini ninaona chapisho hili?”( Why am I seeing this post?) na  “Kwa nini ninaona tangazo hili?” (Why am I seeing this ad). Ikiwa na maana kuwa yanashughulikia kuchambua aina ya matangazo na habari zinazoingia kwenye ukurasa wa watumiaji.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Meneja wa bidhaa wa matandao huo,  Ramya Sethuraman inaeleza kuwa wamezindua “Kwa nini ninaona chapisho hili?”( Why am I seeing this post?) ili kuwasaidia kurasa za watumiaji wa mtandao huo kudhibiti kwa urahisi  habari kutoka kwenye kurasa za marafiki au makundi ya mtandao huo.


Zinazohusiana: 


Akizungumzia maboresho ya “Kwa nini ninaona tangazo hili?” (Why am I seeing this ad) amesema ni zana iliyozinduliwa mwaka 2014 ambapo imeboreshwa baada ya kupokea maoni kutoka kwa watumiaji wao kuhusu usumbufu wa matangazo wanaoupata katika kurasa zao. 

Kwa maboresho hayo, mtumiaji atajua kwa undani kuhusu matangazo ya kibiashara yanayokuja katika ukurasa wake na kama hajaridhishwa anaweza kuchukua hatua muhimu ikiwemo kudhibiti matangazo yasitokee tena katika ukurasa wake.

Ili kupata huduma hiyo mtumiaji wa App hiyo atalazimika kwenda sehemu ya kulia ya ukurasa wake ambayo matangazo na habari kutoka makundi mbalimbali huwekwa na atajulishwa sababu za kila tangazo analiona. 

Kati hatua nyingine, Facebook yenye   watumiaji zaidi ya 1.5 bilioni imeeleza kuwa inataka kuona watumiaji wake wanakuwa huru wakati wakitumia mtandao huo na kama  misingi ya uendeshaji itakuwa imekiukwa wanaweza kuchukua hatua. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV