Emirates yaanza kutumia “Facial Recognition” ukaguzi wa abiria

September 25, 2019 12:02 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni teknolojia ya utambuzi wa sura (Facial Recognition)  ili kuhakiki taarifa za wasafiri wanaotumia ndege hizo.
  • Itasaidia kuondoa usumbufu wa kukagua hati za kusafiria pamoja na kupunguza muda ambao abiria anatumia kukaguliwa. 

Dar es Salaam. Shirika la ndege la Emirates limeanza kutumia teknolojia ya utambuzi wa sura (Facial Recognition)  ili kuhakiki taarifa za wasafiri wanaotumia ndege hizo, jambo litakalosaidia kuokoa muda wakati wa ukaguzi kwenye viwanja vya ndege. 

Huduma hiyo imeanza kutumika kwa wasafari wanaotumia ndege za shirika hilo wanaotokea Marekani na Dubai.

Majaribio ya teknolojia hiyo inayojulikana kama “Biometric boarding” yalifanywa kwa wateja ambao waliondoka Dubai kuelekea jiji la New York nchini Marekani siku chache zilizopita.

“Matokeo yanatia moyo kwa baadhi ya wateja wetu kuingia kwenye ndege kwa kutumia teknolojia ya kutambua sura kwa asilimia 100. 

Kampuni inategemea kuweka teknolojia hii kwenye vituo vyote nchini Marekani mwisho wa mwaka huu baada ya mipango yote kuwa sawa,” imesomeka sehemu ya taarifa Emirates iliyotolewa Septemba 21, 2019.

Emirates imepiga hatua kiteknolojia na kuwa shirika la kwanza nje ya Marekani kuthibitisha taarifa za mteja kwa teknolojia ya kutambua sura baada ya Marekani kuruhusu matumizi ya teknolojia hiyo kupitia kitengo cha udhibiti cha CBP (Customs Border Protection).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wateja wa shirika hilo wanaotoka Dubai nchini Saudi Arabia kwenda kwenye kituo chochote cha Emirates nchini Marekani wataweza kuchagua kutumia teknolojia hiyo  ya kutambua sura.​

Abiria anapigwa picha na mashine hiyo kisha picha yake inalinganishwa na picha yake iliyopo kwenye taarifa za CBP. Picha| Emirates.

Endapo haduma hiyo itakubalika kutumika kwenye viwanja vyote vya ndege, itasaidia kuondoa usumbufu wa kukagua hati za kusafiria pamoja na kupunguza muda ambao abiria anatumia kukaguliwa kwani teknolojia hii inatumia chini ya sekunde mbili kuhakiki taarifa.

Teknolojia hii inafanya kazi kwenye geti la kuingilia kwenye ndege (boarding gate) ambapo abiria anapigwa picha na mashine hiyo kisha picha yake inalinganishwa na picha yake iliyopo kwenye taarifa za CBP. 

Kwa ajili ya usalama wa abiria, kampuni ya Emirates imesema haitatunza taarifa zozote za kibayometriki za abiria bali taarifa hizo zinasimamiwa na CBP. 

Hatua hiyo ni mwendelezo wa kurahisisha usafiri wa ndege na kuwafanya abiria kutokuhitaji makaratasi mengi pale wanaposafiri na haina uandikishaji wowote wa awali unaohitajika. 

Hata hivyo, huduma hiyo siyo ya lazima kwani abiria amepewa uchaguzi kuitumia au kutumia huduma ya kawaida ya ukaguzi wa hati za kusafiria.


Zinazohusiana


Makamu wa Rais wa Idara ya Ulinzi ya Emirates, Dk Abdulla Hashimi amesema kuanzishwa kwa matumizi ya teknolojia hiyo siyo mwisho kwani shirika litaendelea kuboresha huduma zake na kubainisha kuwa “usalama na ulinzi utabaki kuwa kipaumbele” cha shirika hilo.

Wakati teknolojia hiyo ikionyesha mwanzo mzuri wa kuwarahisisha huduma za usafiri wa anga, baadhi ya watumiaji hasa ambao hawajawahi au hawajatembelea Marekani kwa muda mrefu itawapa changamoto kutumia mfumo huo kwa sababu taarifa za hazitapatikana kwenye kanzidata ya CBP.

Mfanya biashara Mathias Matinde ambaye husafiri kwenda Dubai kufanya manunuzi kwaajili ya bidhaa za duka lake amesema teknolojia hiyo itasaidia kwenye kupunguza foleni za ukaguzi wakati wa kupanda ndege. 

“Sijajua kama teknolojia hii itafika Tanzania lakini endapo itafanikiwa basi foleni ya ukaguzi itapungua. kama inachukuia chini ya sekunde mbili hiyo inamaanisha ndani ya dakika moja takribani watu 20 au zaidi watakua wamekaguliwa,” amesema Matinde.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV