‘Dubai Airport’ yaanzisha huduma mpya kwa watoto
- Wamewekewa chumba maalum cha kumpumzikia chenye vifaa mbalimbali vya burudani.
- Lengo ni kuwahakikishia usalama wao wanapotumia uwanja huo wa ndege.
- Wanahudumiwa na watalaam mbalimbali wenye uzoefu wa huduma za ndege.
Watoto wanaosafiri pekee yao kwa kutumia usafiri wa ndege, sasa hawatakua na hofu ya usalama wao wanapokuwa safarini baada ya kuanzishwa kwa chumba maalum cha kupumzikia watoto katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai.
Watoto hao ni wale wanaotoka nchi mbalimbali duniani na wanaosafiri bila kuwa na usaidizi wa wazazi au walezi.
Chumba hicho kimejengwa na kinaendeshwa na kampuni inayotoa huduma za ndege ya dnata kwa ajili ya watoto wanaosafiri peke yao kwa kuwapatia mazingira salama na ya kuvutia wakati wanasubiri ndege katika uwanja huo.
Katika chumba hicho kinachofanya kazi kwa saa 24, kimewekewa runinga na vifaa vya michezo mbalimbali ili kuwaburudisha watoto wanaosafiri, jambo linalowafanya wasichangamane na wasafiri wengine.
Kwa mujibu wa dnata, chumba hicho kinasimamiwa na wahudumu wenye uzoefu na uwezo wa kuongea lugha mbalimbali ili kuhakikisha watoto wanaofika hapo wanahudumiwa vizuri na kupata ndege kwa wakati.
Chumba hicho kimejengwa baada ya dnata kubaini kuwa kuna ongezeko la watoto wanaosafiri bila kuwa na wazazi wao.
Zinazohusiana:
- Mkimbizi wa zamani wa Afghan azunguka Dunia kwa ndege
- Mambo unayotakiwa kuyafanya ukifika mapema “Airport”
Mwaka 2018, timu ya dnata ambayo inatoa huduma za chakula mtandaoni, kuwasaidia wasafiri na kubeba mizigo iliwasaidia watoto 8,000 katika uwanja wa ndege wa Dubai waliokuwa wanasafiri peke yao.
dnata inaeleza kuwa idadi hiyo ya watoto ni ongezeko la asilimia 27 ukilinganishwa na watoto waliohudumiwa miaka mitano iliyopita katika uwanja huo.
Kampuni hiyo ya kimataifa inawahudumiwa watoto wanaosafiri bila wazazi au walezi wanaotumia viwanja viwili vya ndege nchini Dubai kwa kushirikiana na mashirika ya ndege zaidi ya 120 duniani.
Latest
