Dola yapanda kidogo Julai, Euro na Pauni zashuka kulinganisha na Juni

July 1, 2026 8:32 am · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Wafanyabiashara watalazimika kutoboa mifuko zaidi mwanzoni mwa mwezi Julai kulinganisha na mwezi mwanzoni mwa Juni.

Dar es Salaam. Dola ya Marekani imeanza mwezi ikiwa imeimarika kidogo dhidi ya Shilingi ya Tanzania ikilinganishwa na mwanzo wa Juni, huku sarafu kubwa za Ulaya zikiwamo Euro na Pauni ya Uingereza zikionyesha kushuka kwa kiwango kikubwa.

Kwa mujibu wa takwimu za viwango vya kubadili fedha Dola imeongezeka kutoka Sh2,585 mwanzo mwa mwezi Juni hadi Sh2,590 mwanzoni mwa mwezi huu, huku kiwango cha kuuza kikipanda kutoka Sh2,665 hadi Sh2,670 katika benki ya CRDB.

Kwa upande wa NMB, kiwango cha kununua kimeshuka kidogo kutoka Sh2,585 hadi Sh2,580, lakini kiwango cha kuuza kimeshuka pia kutoka Sh2,665 hadi Sh2,660. 

Hii ina maanisha kuwa wafanyabiashara wanaotumia dola kufanya shughuli zao pamoja na kuagiza bidhaa kutoka nje watalazimika kutoboa mifuko yao zaidi mwanzoni mwa mwezi huu kulinganisha na mwezi uliopita.

Mabadiliko hayo yanaendana na mwenendo wa soko unaoonyesha kuwa Shilingi ya Tanzania imeendelea kuwa tulivu, licha ya mabadiliko madogo ya kila siku yanayotokana na nguvu za soko la fedha za kigeni. 

Kwa sarafu za ukanda wa Afrika Mashariki, Shilingi ya Kenya imeimarika kidogo CRDB, ambapo kiwango cha kununua kimeongezeka kutoka Sh16.72 hadi Sh16.78, na kiwango cha kuuza kutoka Sh23.72 hadi Sh23.78. NMB haikuonyesha mabadiliko kwenye viwango vyake vya Shilingi ya Kenya. 

Aidha, Shilingi ya Uganda imeonyesha mabadiliko madogo, hali inayoashiria utulivu wa sarafu hizo katika kipindi hicho. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
2 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
2 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Msikie Jaji Mkuu Masaju : Mambo wasiopaswa kufanya madalali wa Mahakama.

Msikie Jaji Mkuu Masaju : Mambo wasiopaswa kufanya madalali wa Mahakama.

Nukta TV

Dk Mwigulu: Kama siyo Rais Magufuli mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere usingefanyika

Dk Mwigulu: Kama siyo Rais Magufuli mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere usingefanyika

Nukta TV

Umuhimu wa elimu ya mikopo

Umuhimu wa elimu ya mikopo

Nukta TV