Deni la Serikali laongezeka kwa Sh8 trilioni ndani ya mwaka mmoja

June 14, 2022 8:25 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ongezo la deni hilo limetokana na kupokelewa kwa mikopo mipya kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. 
  •  Tathmini zinasema deni  la Serikali bado ni himilivu.

Dar es Salaam. Deni la Serikali limeongezeka kwa zaidi ya Sh8 trilioni ndani ya mwaka mmoja likichochewa na kupokelewa kwa mikopo mipya kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba ameliambia Bunge leo kuwa deni hilo la Serikali lilifikia  Sh69.44  trilioni Aprili 2022 kutoka na Sh60.72 trilioni kipindi  kama hicho mwaka 2021 ikiwa ni sawa na ongezeko  la asilimia 14.4.

Kwa hesabu hizo, deni la Serikali liliongezeka kwa Sh8.72 trilioni ndani ya mwaka mmoja. 

“Kati ya  kiasi hicho, deni la nje lilikuwa shilingi trilioni 47.07 na deni la ndani  lilikuwa Sh22.37 trilioni,” amesema Dk Nchemba wakati akiwalisha Bungeni taarifa ya hali ya uchumi wa taifa  kwa mwaka 2021 na mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka 2022/2023

Ongezeko la deni hilo, amesema  lilitokana na  kupokelewa kwa mikopo mipya kutoka vyanzo vyenye masharti nafuu na ya kibiashara kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo.

“Aidha,  ongezeko la deni limetokana na kutolewa kwa hatifungani maalumu  yenye thamani ya Sh2.18 trilioni kwa ajili ya deni la Mfuko wa  Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) lililotokana na  michango ya watumishi wa kabla ya mwaka 1999,” amesema Dk Nchemba.

Licha ya ongezeko la deni hilo, waziri huyo amesema taarifa ya tathmini  ya uhimilivu wa deni iliyofanyika Novemba 2021 inaonesha kuwa deni  la Serikali bado ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na  mrefu kwa kuzingatia ukomo wa viashiria vyote vinavyokubalika  kimataifa. 

Hata hivyo, kumekuwa na msukumo mkubwa miongoni mwa wadau wa maendeleo ambao wamekuwa wakionya juu ya kasi ya ongezeko la deni la Serikali ndani ya miaka mitano iliyopita.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV