DCEA yakamata zaidi ya tani 37 za dawa za kulevya

July 9, 2025 5:47 pm ยท Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Raia wa kigeni wahusika, maiti kuanza kutumika tena, DCEA yasema watanzania wanahatarishwa kutumika kama wasafirishajiย 

Dar es salaam. Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imekamata dawa za kulevya zenye uzito wa jumla ya kilogramu 37,197.1 katika operesheni zilizofanyika nchi nzima kati ya Mei na Julai 2025.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo leo Julai 9,ย  dawa hizo zinajumuisha kilogramu 11,031.42 za dawa mpya ya kulevya ya Mitragyna Speciosa (inayojulikana kama Kratom),ย 

Dawa hizo ziliingizwa nchini kutokea Sri Lanka zilikamatwa katika maeneo ya bandari iliyoko Temeke jijini Dar es Salaam zikiwa kwenye vifungashio vyenye chapa inayoonesha kuwa ndani yake kuna mbolea.

Kwa mujibu wa ufafanuzi uliotolewa na DCEA, Mitragyna speciosa iko katika kundi la dawa mpya za kulevya zinazotokana na mimea inayofahamika kwa jina la โ€œKratomโ€ ambaoย  unakemikali yenye sifa ya vichangamshi (stimulants) na vipumbaza (depresants) vyenye madhara ya kiafya kwa mtumiaji.

DCEA imesema miongoni mwa athari ni pamoja na kuathirika kwaย  mfumo wa fahamu, kusababisha uraibu na hata kusababisha vifo vya ghafla.

Aidha, katika oparesheni hiyo iliyohusisha vyombo vingine vya dola, DCEA ilikamata bangi kilogramu 24,873.56, mirungi kilogramu 1,274.47, skanka kilogramu 13.42, heroin kilogramu 2.21 na methamphetamine gramu 1.42.ย 

โ€œPia, dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya ketamine kilogramu 1.92, vidonge 1,000 vya flunitrazepam (maarufu kama rohypnol) na lita 6 za kemikali bashirifu aina ya hydrochloric acid zilinaswa,โ€ imeeleza taarifa ya DCEA.

Wakati huo huo, DCEA imesema ilibaini kiwanda bubu katika eneo la Sinza jijini Dar es Salaam kilichokuwa kikizalisha biskuti zilizochanganywa na bangi na kusambaza bidhaa hizo katika mikoa ya Mwanza, Lindi na Mtwara ambapo mfanyabiashara mmoja wa madini mkoani Lindi alikamatwa akisambaza biskuti hizo.

Raia wa kigeni watajwa

Aidha, DCEA imebaini uwepo wa matukio ya raia wa kigeni kuwatumia Watanzania kusafirisha au kusambaza dawa za kulevya kwa kuanzisha mahusiano ya kirafiki na kisha kuwahusisha katika biashara hiyo kwa kutumia kampuni za wazawaย  na vyombo vyao vya usafiri hususani bodaboda, bajaji, Tax na wasambazaji wa vifurushi.

Mitragyna speciosa iko katika kundi la dawa mpya za kulevya zinazotokana na mimea inayofahamika kwa jina la โ€œKratomโ€ ambaoย  unakemikali yenye sifa ya vichangamshi (stimulants) na vipumbaza (depresants) vyenye madhara ya kiafya kwa mtumiaji. Picha | Britanica.

DCEA imetoa wito kwa wananchi kuwa makini na kujiridhisha kabla ya kusafirisha au kupokea mzigo kutoka kwa watu wasiowafahamu vizuri, kwa kuwa mizigo hiyo huenda ikawa sehemu ya mtandao wa usafirishaji wa dawa za kulevya bila wao kujua.

Hata hivyo, mamlaka imebaini kuwa baadhi ya wahalifu wa dawa za kulevya wameanza tena kutumia maiti za binadamu kubeba dawa za kulevya, maarufu kwa jina la begi.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW