Corona kuhatarisha ajira bilioni 1.6 duniani

April 30, 2020 6:08 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni ajira katika sekta isiyo rasmi ambazo karibu nusu ya wafanyakazi wote duniani.
  • Hiyo inatokana na kupungua kwa saa za kazi na mapato. 

Ripoti mpya zilizotolewa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) inaeleza kuwa kuendelea kupungua kwa saa za kazi kutokana na athari za virusi vya Corona (COVID-19) kunazidi kuhatarisha ajira katika sekta isiyo rasmi ambayo ni karibu nusu ya wafanyakazi wote duniani.

 Ripoti hiyo iliyotolewa jana kuhusu athari za virusi vya corona au COVID-19 katika soko la ajira (ILO Monitor third edition: COVID-19 and the world of work) inaeleza kuwa athari za COVID-19 zinawaweka katika sintofahamu wafanyakazi  bilioni 1.6 wa sekta zisizo rasmi za kiuchumi na kwa mamilioni ya makampuni duniani. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kupungua kwa saa za kazi katika robo ya pili ya mwaka 2020 kumechangia hali hiyo na kunatarajiwa kuwa kubaya zaidi ya ilivyokadiriwa hapo awali.

Ikilinganishwa na robo ya nne ya mwaka 2019 kabla ya kuzuka kwa janga la Corona hivi sasa inatarajiwa kuwa ajira zitashuka kwa asilimia 10.5 sawa na ajira milioni 3.5 za kutwa nzima ambazo watu hufanya kazi ya saa 48 kwa wiki.


Soma zaidi: 


ILO inasema hapo awali makadirio yalikuwa ajira kushuka kwa asilimia 6.7 sawa na wafanyakazi wa kutwa nzima milioni 195 na hii ni kutokana na kuongezwa kwa muda wa watu kujitenga na kusalia majumbani.

Hiyo ina maana kuwa wafanyakazi bilioni 1.6 kutoka uchumi usio rasmi kati ya jumla ya ajira bilioni mbili na wafanyakazi bilioni 3.3 duniani kote wameathirika katika kiwango cha kupata mapato ya kuwawezesha kuishi.

“Hii imetokana na hatua za kuzuia kusambaa kwa maambukizi au ni kwa sababu wanafanya kazi katika sekta ambazo zimeathirika Zaidi na janga hili,” inaeleza ripoti hiyo. 

ILO imetaka juhudi za kupambana na virusi hivyo ziimarishwe huku mikakati ya kuokoa ajira za watu nayo ibuniwe ili kuwapa ahueni wafanyakazi. 

Enable Notifications OK No thanks