“Can You Keep a Secret?”: Filamu inayofungua pazia kwa wasiopenda kutunza siri zao 2020

January 3, 2020 11:12 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Filamu ya “Can You Keep a Secret?” inaonyesha sekeseke la mapenzi na uwezo wa kutunza siri.
  • Fahamu jinsi mazoea kwenye mahusiano yanavyoweza kumkwaza mpenzi wako.
  • Hata baada ya  kumwaga siri zake za chumbani, bado Jack anamchagua Emma.

Dar es Salaam. Huenda kisa hiki kikakukumbusha historia inayofanana na ya kwako kama ukikumbuka vizuri. Je,umewahi kutoa siri zako kwa mtu ambaye hata humfahamu? 

Kama ndiyo, kisa chako kinafanana na cha Emma Corrigan ambaye anajikuta akitoa siri zake za ndani kwa Jack Harper ambaye amekutana naye kwa mara ya kwanza kwenye ndege wakiwa wanasafiri pamoja.

Kisa hicho kilichopo kwenye filamu ya “Can You Keep a Secret?” kinaelezea jinsi mawazo na sintofahamu ya maisha ya kimapenzi ya Emma yanamfanya kunywa pombe nyingi akiwa kwenye ndege na kujikuta akitoa siri za chumbani kwa jirani yake Jack.

Hata hivyo, kumwaga siri kulianza baada ya ndege waliyopanda kutaka kuanguka lakini mambo yanabadilika kwa Emma baada ya ndege hiyo kutua bila hata mkwaruzo.

Ndiyo, Najua unajiuliza kama Emma aliweza kumtizama Jack usoni au laa baada ya ndege kuwasiri ilipokusudiwa. Lakini jaribu kujiuliza hali yake inakuwaje baada ya Jack kutangazwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya  wa ofisi ambayo Emma anafanyia kazi?


Zinazohusiana


Je ataweza kuendelea na kazi ikiwa bosi wake anafahamu A-Z ya maisha yake yote? Jibu swali hilo huku ukiona jinsi taratibu Emma na Jack wanakua wapenzi wanaopitia milima na mabonde kwenye safari yao ya mahaba.

Unakosaje kuangalia kisa hiki matata kilichoongozwa na Elise Duran ambaye ameongoza filamu nyingi zikiwemo za  “Why I Ran” na “My Rescue”

Anza mwaka wako na filamu hii ambayo inaonyeshwa kenye kumbi za sinema za Century Cinemax kwenye maduka makubwa ya manunuzi (Malls) yakiwemo ya Mlimani City na Dar Free Market.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
18 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
19 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
19 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV