Bei ya wanyamapori yagonganisha vichwa mawaziri Afrika

September 8, 2021 7:59 am · Medlini
Share
Tweet
Copy Link

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro akizungumza na jambo na Waziri wa Utalii wa Gambia, Hamat Bah  mara baada ya  Mkutano wa  Kimataifa wa  64 wa Utalii Kanda ya Afrika  ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaoendelea  kufanyika katika kisiwa cha SAL nchini Cape Verde.


  • Ni kutokuwa na bei zinazolingana za wanyama hao.
  • Imesababishwa nchi za Afrika kukosa mapato.
  • Afrika yajipanga kutoa msimamo wa pamoja.

Dar es Salaam. Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Damas Ndumbaro  amezitaka nchi za Afrika kuwa na kauli moja kuhusu taratibu na bei za wanyamapori katika biashara ya uwindaji wa kitalii.

Dk Ndumabara ametoa wito huo alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti katika vikao  vya ana  kwa ana na baadhi ya  mawaziri wa utalii wa nchi za Afrika katika mkutano wa 64 wa  kimataifa wa utalii uliondaliwa na Shirika la Umoja wa Kimataifa la Utalii Duniani  (UNWTO) unaofanyika kwa muda wa siku nne nchini Cape Verde.

“Utofauti wetu huu umekuwa ukitukandamiza kama nchi kwani tulitakiwa sisi ndio tupange bei lakini kutokana na kutokuwa na umoja bei za wanyama zimekuwa zikiamuliwa na wao hili lazima tulikatae kwa kuungana kwa pamoja,” amesema Dk Ndumbaro.

Amezitaka nchi zote zinazoendesha utalii wa uwindaji zifanye mkutano kwa njia ya mtandao ili kujadili mustakabali wa biashara hiyo na kisha  zitoke na kauli moja ili kuwathibiti wawindaji wa kitalii kwa ajili ya maslahi mapana ya uhifadhi barani Afrika.

Nchi zinazofanya vizuri katika uwindaji wa kitalii ni pamoja na Botswana, Zimbabwe, Tanzania, Zambia na Afrika Kusini

Kauli hiyo imeungwa mkono na Waziri wa Utalii wa Zimbabwe, Ngoghithize Ndlovu na amezitaka nchi hizo kuwa kitu kimoja katika kuamua kupanga bei za uwindaji wa kitalii.

Amesema bei za wanyama wanaoruhusiwa kuwindwa pamoja na vitalu vya uwindaji wa wanyamapori zimekuwa zikitofautiana sana kati ya nchi na hali hiyo imekuwa kikwazo kikubwa kwa shughuli uhifadhi barani Afrika.

Kutokana na kutofautiana kwa bei na baadhi  ya kanuni na taratibu hizo, wawindaji wa kitalii wamekuwa wakitumia mwanya huo  kuzikandamiza nchi za Afrika kwa kupanga bei wanazotaka wao huku wakidai kuwa bei hizo cha chini zimekuwa katika nchi nyingine pia.

Katika hatua nyingine,  Dk Ndumbaro ametoa ahadi kwa Zimbabwe  kama itakuwa  tayari ipewe mafunzo ya kuendesha biashara ya uwindaji wa kitalii kwa mfumo wa digitali ambao utasaidia kuongeza mapato katika nchi hiyo.

Amesema tangu kuanzishwa kwa mfumo huo nchini Tanzania umeleta manufaa makubwa kwa nchi  ambapo wawindaji wa kitalii ili kuweza kupata vitalu vya uwindaji wamekuwa wakilazika kushiriki katika mnada wa kimtandao.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV