Asilimia 0.2 waliojiunga JKT wakutwa na VVU

February 5, 2023 6:51 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

  • Vijana 147 kati ya 67,299 waliojiunga na jeshi hilo kati ya 2019 na 2021 walikutwa na VVU.
  • Kamati ya Bunge yashauri elimu iongezwe miongoni mwa vijana.

Dar es Salaam. Asilimia 0.2 ya vijana waliojiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika kipindi cha miaka mitatu wamekutwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi ya Februari 2022 hadi Februari 2023 iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma Februari 3 mwaka huu imeeleza kuwa vijana 147 kati ya 67,299 waliojiunga na jeshi hilo miaka mitatu walikutwa na VVU.

Vijana hao ni wale waliomaliza kidato cha sita ambao walijiunga na JKT kati ya mwaka 2019 na 2021. 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwaka 2019, vijana waliojiunga JKT walikuwa 20,413 ambapo kati yao 60 walikutwa na maambukizi wakati 2020 walijiunga vijana 21,383 na maambukizi yalikuwa kwa vijana 45.

Mwaka 2021 walijiunga vijana 25,503 na 42 kati yao ndiyo walikutwa na VVU.

Kamati hiyo katika taarifa yake imependekeza mkakati wa kupima na kuzuia maambukizi mapya ya VVU uongezwe.

Enable Notifications OK No thanks