Ahueni, maumivu: Startups za Tanzania wakati wa Uviko-19

November 4, 2021 2:03 pm · Herimina
Share
Tweet
Copy Link
  • Asilimia 70 ya startups zinapata changamoto ya kujiendesha baada kupungua kwa mapato
  • Startups 3 kati ya 10 zimeimarika wakati wa janga la Uviko-19.
  • Wadau washauri kupunguza kodi na kuanzisha mfuko wa kuzisaidia startups ili usaidie kutunisha mitaji yao. 

Dar es salaam. Tangu kuanza kwa janga la Uviko-19 nchini Tanzania, utendaji wa kampuni zinazochipukia (Startups) umeathirika kutokana na changamoto na athari za ugonjwa huo huku baadhi zikishindwa kabisa kufanya shughuli zake.

Ripoti ya Chama cha Kampuni zinazochipukia Tanzania (TSA) kuhusu athari za Uviko-19 ya mwaka 2020, inaonyesha kuwa asilimia 65 au ya startups za Tanzania  mapato yake yalipungua kwa zaidi ya asilimia 50. Hii ina maani kuwa startups mbili kwa kila tatu zilizopo Tanzania zilipoteza nusu ya mapato yake kutokana na Uviko-19, jambo lililorudisha nyuma safari ya ukuaji wa kampuni hizo na kupunguza mchango wao katika ukuaji wa uchumi. 

Vilevile, asilimia 2.5 ya startups zinazojihusisha na uingizaji na usafirishaji bidhaa nje ya nchi zilishindwa kufanya shughuli zake kutokana na vikwazo vya usafiri kukabiliana na Uviko-19. Maoema mwaka jana baada ya Uviko-19 kuingia katika mataifa mbalimbali ulimwenguni mipaka ilifungwa kiasi cha kuathiri zaidi sekta ya usafirishaji na utalii. 

Licha ya changamoto hizo, ripoti hiyo iliyotolewa hivi karibuni inaonesha kuwa “startups” 3 kati ya 10 zimeimarika huku asilimia 30 ya kampuni hizo zikipata ongezeko la mapato katikati ya janga la uviko-19. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV