Pauni na Euro zaendelea kuimarika dhidi ya Shilingi ya Tanzania

November 3, 2026 9:05 am · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Dola ya Marekani na sarafu zingine za kigeni zaendelea kuwa tulivu.

Dar es Salaam. Pauni ya Uingereza pamoja na sarafu ya Umoja wa Ulaya (Euro) zimeonesha kupanda ukilinganisha viwango vilivyotumika jana kufuatia ongezeko la thamani ya sarafu hizo katika viwango vya ubadilishaji fedha vilivyotelewa leo Novemba 3, 2026 na benki za CRDB na NMB.

Kwa mujibu wa benki ya CRDB Euro imenunuliwa kwa Sh2,817.15 na kuuzwa kwa Sh3,117.15 kutoka bei iliyotumika jana ya kununua kwa Sh2,802.58 na kuuzwa kwa Sh3,102.58 ikiwa ni sawa na ongezeko la Sh14.57 mtawaliwa.

Kwa upande wa benki ya NMB leo imenunua Euro kwa Sh2,790 na kuuza kwa Sh3,087 ukilinganisha na siku ya jana ambapo Euro ilinunuliwa kwa Sh2,780 na kuuza kwa Sh3,076 sawa na ongezeko la Sh10 kwa bei ya kununua na viwango vya kuuza ikiongezeka kwa Sh11.

Pauni ya Uingereza katika benki ya CRDB leo inanunuliwa kwa Sh3,399.79 na kuuzwa kwa Sh3,699.79 huku NMB ikinunuliwa kwa Sh3,333 na kuuzwa kwa Sh3,687.

Bei hizo zilizotumika leo ni sawa na ongezeko Sh6.94 kwa bei ya kununua CRDB na Sh3 kwa bei ya kununua NMB.

Dola ya Marekani imeendelea kuwa tulivu kwa kusalia katika viwango vile vile vya biashara, hali inayoonyesha utulivu wa mahitaji ya sarafu hiyo katika soko la kigeni nchini.

Kwa siku za hivi karibuni sarafu ya Euro imekua ikionesha mabadiliko kutokana na kupanda na kushuka kwa sarafu hiyo dhidi ya shilingi ya Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
3 Nov, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
3 Nov, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Maelekezo ya Rais Samia kwa Tume ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kazi

Maelekezo ya Rais Samia kwa Tume ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kazi

Nukta TV

Rais Samia aitaka Tume ya Haki za Binadamu kujibu shutuma dhidi ya Tanzania

Rais Samia aitaka Tume ya Haki za Binadamu kujibu shutuma dhidi ya Tanzania

Nukta TV

Rais Samia aagiza manne, mji wa Serikali, Mtumba

Rais Samia aagiza manne, mji wa Serikali, Mtumba

Nukta TV