Tanzania, Angola kuimarisha biashara na usafirishaji 

October 29, 2026 5:12 pm · Method Allen
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni fursa kwa wananchi kutumia ushirikiano huo unaotarajiwa kurahisisha usafiri wa watu na bidhaa pamoja na kukuza biashara kukuza kipato binafsi na kuchechemua uchumi wa nchi.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania na Angola zimesaini mikataba minne ya makubaliano kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kupitia sekta za biashara na usafirishaji hatua inayolenga kuongeza uwekezaji na utalii kwa mataifa hayo mawili.

Hatua hiyo imefikiwa leo, Oktoba 29, 2026, Ikulu jijini Dar es Salaam, baada ya mazungumzo kati ya Rais Samia Suluhu Hassan na Rais  João Lourenço wa Angola, kufuatia ziara yake ya siku tatu ya kikazi nchini.

Akizungumza mara baada ya makubaliano Rais Samia amesema  ushirikiano huo unahusisha ukarabati wa reli ya Tazara upande wa Tanzania na reli ya Benguela inayopitia Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Zambia kwa upande wa Angola.

Mbali na mambo mengine, marais hao wawili wamekubaliana kufungua tena ubalozi wa Tanzania nchini Angola ili kuendelea kudumisha uhusiano wa kihistoria na kidugu uliopo kati ya Angola na Tanzania, pamoja na kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi ili kuchochea maendeleo ya mataifa yote kwa maslahi ya wananchi | Picha Ikulu Mawasiliano

Amesema miradi hiyo inalenga kuunganisha ukanda wa Lobito na ukanda wa kati unaounganisha na Bandari ya Dar es Salaam ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na kukuza biashara. 

“Moja wapo wapo ya kikwazo kikubwa cha biashara barani Afrika ni changamoto ya miundombinu ya usafiri na usafirishaji, hivyo tumekubaliana kutatua changamoto hii kwa kuunganisha korido za Lobito na Dar es Salaam,” amesema Rais samia. 

Fursa kwa Watanzania 

Hii ni kwa mara ya kwanza Rais Lourenço kutembelea Tanzania tangu Rais wa kwanza wa Taifa hilo, Agostino Neto alipofanya hivyo mwaka mwaka 1979 wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika.

Ujio wake na makubaliano haya mapya ni fursa kwa wananchi kutumia ushirikiano unaotarajiwa kurahisisha usafiri wa watu na bidhaa pamoja na kukuza biashara, uwekezaji na utalii kati ya Tanzania na Angola kuongeza kipato binafsi na kuchechemua uchumi baina ya mataifa hayo.

Kwa upande wake Rais Lourenço ametoa wito kwa kwa mataifa mengine ya Afrika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi ndani ya bara ili kutumia fursa zilizopo na kupunguza utegemezi mkubwa wa biashara na uwekezaji kutoka Ulaya, Amerika na Asia. 

“Tumekua tukiacha uhusiano na nchi zetu ambazo ni ndugu, nchi za Kiafrika ambazo zina kitu cha kuweza kusaidia katika kuleta maslahi ya pamoja, ambapo wote tunaweza kunufaika,” amesema Rais Lourenço

Mbali na mambo mengine, marais hao wawili wamekubaliana kufungua tena ubalozi wa Tanzania nchini Angola ili kuendelea kudumisha uhusiano wa kihistoria na kidugu uliopo kati ya Angola na Tanzania, pamoja na kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi ili kuchochea maendeleo ya mataifa yote kwa maslahi ya wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
29 Oct, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
30 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
30 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Makonda: 28 - 30 Oktoba ni siku za kumshukuru Mungu kwa kuitunza amani ya Tanzania

Makonda: 28 - 30 Oktoba ni siku za kumshukuru Mungu kwa kuitunza amani ya Tanzania

Nukta TV

Nape: Mkutano wa IPU umetoa fursa kwa wageni kujionea picha halisi ya Tanzania

Nape: Mkutano wa IPU umetoa fursa kwa wageni kujionea picha halisi ya Tanzania

Nukta TV

Mikoa 10 tajiri zaidi Tanzania 2025

Mikoa 10 tajiri zaidi Tanzania 2025

Nukta TV