BoT yauza tani 5 za dhahabu kuongeza fedha za kigeni 

October 9, 2026 2:28 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Dhahabu hiyo iliuzwa kwa bei ya takribani Dola za Marekani 4,640 kwa wakia moja.

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeuza tani 5.1 za dhahabu kutoka kwenye akiba yake ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kusimamia akiba za taifa na kuongeza fedha za kigeni nchini. 

Kwa mujibu wa Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba, dhahabu hiyo iliuzwa kwa bei ya takribani Dola za Marekani 4,640 kwa wakia moja, baada ya wataalamu wa masoko ya fedha kutathmini mwenendo wa bei na kubaini kuwa wakati huo ulikuwa mwafaka kwa mauzo. 

“Tulikuwa na akiba ya tani 35.4, ambayo tumewahi kununua na kati ya hiyo tumeuza tani 5.1, kwahiyo ukicheki hapo maana yake tuna kama tani 30 hivi,” alisema Tutuba katika mkutano wake na wanahabari jana Oktoba 8,2026.

Tutuba amesema kuwa, mbali na kuongeza fedha za kigeni, ununuzi na uuzaji wa dhahabu unalenga kuimarisha mnyororo wa thamani wa madini hayo na kuchangia uthabiti wa shilingi. 

Kwa mwananchi wa kawaida, akiba ya fedha za kigeni ni muhimu katika kulipia bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, kama mafuta, dawa na mashine, hivyo kuchangia upatikanaji wa bidhaa hizo na kupunguza shinikizo la kushuka kwa thamani ya shilingi. 

Hata hivyo, hatua hiyo haimaanishi moja kwa moja kuwa bei za bidhaa zitashuka au maisha yatakuwa nafuu, kwani hali hiyo hutegemea pia mwenendo wa bei za dunia, gharama za uagizaji na mambo mengine yanayoathiri uchumi. 

Si mara ya kwanza

Hii si mara ya kwanza kwa BoT kutangaza mpango wa kuuza sehemu ya akiba yake ya dhahabu mwaka huu.

Februari 19, 2026, benki hiyo ilieleza mpango wa kuuza sehemu ya dhahabu iliyokusanya ili kusawazisha akiba zake na kuendelea na ununuzi kwa kuzingatia mgao wa kimkakati wa fedha za kigeni.

Mpango huo ulizua mjadala miongoni mwa wananchi kuhusu sababu za benki hiyo kuuza dhahabu iliyokusanya, huku suala hilo likifika hadi Bungeni Juni 18, 2026.

Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba aliliambia Bunge kuwa BoT ilisimamisha mpango huo baada ya bei ya dhahabu katika soko la kimataifa kushuka na kufikia kiwango kilichokuwa chini ya bei ambayo benki hiyo ililenga kuuza. 

‘Tutaendelea kuuza’

Akizungumzia dhahabu iliyobaki kwenye akiba ya benki hiyo, ambayo ni takribani tani 30.3, Tutuba amesema BoT itaendelea kununua na kuuza dhahabu kulingana na mwenendo wa bei katika soko la kimataifa akibainisha kuwa ili benki hiyo ipate faida ni lazima iuze na kununua.

“Hakuna biashara ambayo unanunua tu bila kuuza…kwahiyo tunaendelea kununua na tutaendelea kuuza kulingana na bei inavyoimarika,” amesema Tutuba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
30 Oct, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
30 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
30 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Tanzania na Angola kuunganisha reli na safari za ndege

Tanzania na Angola kuunganisha reli na safari za ndege

Nukta TV

Tanzania kufungua tena ubalozi Angola, Balozi mpya kuteuliwa

Tanzania kufungua tena ubalozi Angola, Balozi mpya kuteuliwa

Nukta TV

Makonda: 28 - 30 Oktoba ni siku za kumshukuru Mungu kwa kuitunza amani ya Tanzania

Makonda: 28 - 30 Oktoba ni siku za kumshukuru Mungu kwa kuitunza amani ya Tanzania

Nukta TV