BoT yarudisha mjadala, ukomo miaka 10 kwa mabosi wa benki, taasisi za fedha 

October 2, 2026 12:29 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Kwa sasa, BoT bado haijafanya rasimu hiyo kuwa kanuni mpya. Imeiweka wazi kwa ajili ya maoni ya umma, huku tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maoni ikiwa Oktoba 28, 2026.

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeibua tena mjadala wa viongozi wakuu na wajumbe wa bodi za benki na taasisi za fedha kung’oka madarakani baada ya kutumikia kwa kipindi cha miaka 10.

Mjadala huo umerejeshwa ikiwa ni takribani miaka mitano tangu ukomo huo uainishwe katika Kanuni za Utawala Bora za mwaka 2021, kabla ya kanuni hizo kufanyiwa marekebisho mwaka 2023.

Kwa mujibu wa Rasimu ya Kanuni za Benki na Taasisi za Fedha ya Usimamizi wa Utawala Bora ya mwaka 2026, iiyotolewa Septemba 28, 2026 maoni yatakusanywa kwa siku 30 hadi kufikia ukomo ambao ni Oktoba 28, 2026.

Hatua hiyo inakuja wakati sekta ya fedha ikiendelea kubadilika kwa kasi kutokana na teknolojia, ushindani wa huduma za kifedha na mahitaji mapya ya wateja, hivyo suala la namna taasisi zinavyopanga mabadiliko ya uongozi linazidi kuwa muhimu.

Si mara ya kwanza 

Hata hivyo, sharti hili la miaka 10 si jipya. Miaka mitano iliyopita BoT ililiweka sharti hilo kwenye kanuni za utawala bora za mwaka 2021, kabla ya kufanya marekebisho.

Kanuni hizo pia ziliweka sharti kwamba mtu aliyefikisha miaka 10 katika taasisi hawezi kurudi kwenye taasisi hiyo au kampuni tanzu yake katika nafasi yoyote hadi ipite miaka mitatu.

Aidha, kwa waliokuwa tayari wamefanya kazi kwa miaka 10 au zaidi wakati kanuni hizo zinaanza kutumika, BoT iliweka kipindi cha mpito cha miaka miwili kabla ya kuacha nafasi zao.

Mwaka 2023, BoT ilifanya marekebisho ya kanuni hizo, lakini marekebisho hayo yalihusu vipengele vingine vya utawala bora na hayakuondoa sharti la miaka 10.

Kwanini miaka 10 ?

Kwa zaidi ya muongo mmoja, kiongozi wa taasisi ya fedha anaweza kuwa amejenga uzoefu, mtandao wa kibiashara na uelewa mkubwa wa taasisi anayoiongoza. 

Lakini swali linalobaki sasa ni je, kwanini BoT inaendelea na sharti hili au kuna umuhimu gani kwa kiongozi kuachia madaraka baada ya muda fulani wa utumishi kwenye taasisi ya fedha ?

Mtaalamu wa fedha na uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Abel Kinyondo, anasema uongozi katika sekta ya fedha unapaswa kuwa wa kiwango cha juu muda wote ili kulinda taasisi na uchumi kwa ujumla.

Anasema mtu anapokaa muda mrefu katika taasisi anaweza kuanza kufanya mambo kwa mazoea badala ya kuendeshwa na misingi ya kitaalamu, au hata kufikia hatua ya kujiona kama sehemu isiyoweza kutenganishwa na taasisi hiyo.

Profesa Kinyondo anasema kuondoa ukomo wa muda wa viongozi wa taasisi za fedha kunaweza kuwa kosa kubwa katika suala la utawala bora, akieleza kuwa kanuni hiyo ni sehemu ya utaratibu unaotumika kimataifa katika kulinda taasisi za fedha dhidi ya hatari za uongozi wa muda mrefu.

“Benki ikianguka, uchumi unatikisika. Huwezi kumwacha mtu mmoja kuwa kama tembo kwenye kampuni,” anasisitiza Profesa Kinyondo.

Anaeleza kuwa baada ya kiongozi kukaa zaidi ya miaka 10, hata bodi iliyokuwa ikimsimamia inaweza kuwa imebadilika na nafasi yake kuchukuliwa na bodi mpya ambayo inaweza kukutana na kiongozi mwenye uzoefu mkubwa kuliko wajumbe wapya.

“Mtu akikaa zaidi ya miaka 10, maana yake hata ile bodi iliyokuwa inamsimamia itakuwa imemaliza muda, inakuja bodi nyingine. Bodi mpya inapokuja ikakuta mtu ana zaidi ya miaka 10, hiyo bodi haina uwezo wa kumwambia kitu chochote huyo bwana,” anasema Profesa Kinyondo.

Mchumi huyo ameongeza kuwa  hakuna hatari kubwa katika kubadilisha viongozi baada ya kufikisha muda uliowekwa, kwa kuwa taasisi inaweza kuandaa mapema viongozi wengine wenye uwezo wa kushika nafasi hiyo au kutangaza nafasi na kupata kiongozi mpya.

Kwa sasa, BoT bado haijafanya rasimu hiyo kuwa kanuni mpya. Imeiweka wazi kwa ajili ya maoni ya umma, huku tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maoni ikiwa Oktoba 28, 2026.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
2 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
2 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Zingatia mambo haya kabla ya kusaini mkataba wa ajira

Zingatia mambo haya kabla ya kusaini mkataba wa ajira

Nukta TV

Rasmi wageni kuanza kulipa USD44, bima ya safari Tanzania

Rasmi wageni kuanza kulipa USD44, bima ya safari Tanzania

Nukta TV

Hofu yatajwa, kwanini Watanzania wengi hawapimi afya mara kwa mara?

Hofu yatajwa, kwanini Watanzania wengi hawapimi afya mara kwa mara?

Nukta TV