Himanshu Shekhar, bosi mpya SBC Tanzania

September 4, 2026 4:58 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Shekhar anakalia kiti cha CEO wakati SBC Tanzania ikikabiliwa na ushindani kutoka kwa wazalishaji na wasambazaji wengine wa vinywaji, akiwemo Coca-Cola Kwanza, kampuni tanzu ya Coca-Cola Beverages Africa (CCBA).

Dar es Salaam. Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya SBC Tanzania Limited, imemteua Himanshu Shekhar kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kampuni hiyo inayozalisha na kusambaza vinywaji vilivyopo chini ya nembo ya Pepsi nchini.

Uteuzi huo uliotangazwa leo Septemba 4, 2026, unamkutanisha Shekhar na jukumu la kuongoza SBC Tanzania katika kipindi ambacho kampuni hiyo inaendelea kupanua uwezo wake wa uzalishaji na mtandao wa biashara nchini.

Bosi huyo mpya pia anaingia katika kipindi ambacho soko lina ushindani mkubwa katika bidhaa za soda na vinywaji vingine baridi. 

Katika miaka 10 ya hivi karibuni Tanzania imeshuhudia ongezeko kubwa la wazalishaji wa soda na juisi kiasi cha kufanya kila mzalishaji kupambana kuongeza wigo la watumiaji wa bidhaa zao. 

Kabla ya kuteuliwa kuwa CEO, Shekhar alikuwa akihudumu kama Mkuu wa Uendeshaji (COO) wa SBC Tanzania, nafasi aliyopandishwa na kampuni baada ya kuonesha uwezo katika uongozi wa shughuli za kampuni na utekelezaji wa mikakati ya biashara. 

SBC imeeeleza kuwa kupandishwa kwake kuwa COO kulitokana na uongozi wake katika shughuli za uendeshaji, uwezo wa kutekeleza mipango na kujitolea kwake kwa kampuni.

Katika kipindi chake kama COO, Shekhar alishiriki moja kwa moja katika shughuli za uzalishaji na uendeshaji wa vituo vya kampuni katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo Mwanza, Arusha na Kilimanjaro.

SBC Tanzania, iliyoanzishwa miaka 25 iliyopita, ni sehemu ya biashara ya familia ya El-Khalil, ambayo historia yake katika biashara ya vinywaji inaanzia Seven-Up Bottling Company ya Nigeria. 

Kampuni hiyo ndiyo mtengenezaji na msambazaji wa bidhaa za Pepsi nchini Tanzania, ikiwa na viwanda vinne vilivyopo Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya.

Kijiti cha kukuza biashara

Uteuzi wa Shekhar unakuja wakati SBC Tanzania ikiendelea kuongeza uwezo wake wa uzalishaji katika safari yake ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwake.

Katika maadhimisho ya miaka 25 ya kampuni, uongozi wa SBC Tanzania ilitangaza mipango ya kuongeza kiwanda na uzalishaji katika kiwanda cha Arusha pamoja na kujenga kiwanda kipya mkoani Dodoma.

Aidha ilitangaza mkakati wa kuongeza uwezo wa uzalishaji wa chupa za PET, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kukidhi mahitaji ya soko na kuongeza upatikanaji wa bidhaa zake. 

Shekhar anakalia kiti cha CEO wakati SBC Tanzania ikikabiliwa na ushindani kutoka kwa wazalishaji na wasambazaji wengine wa vinywaji, akiwemo Coca-Cola Kwanza, kampuni tanzu ya Coca-Cola Beverages Africa (CCBA). Picha | Shekhar | LinkedIn

Hivyo, Shekhar anakalia kiti cha CEO akiwa na jukumu la kusimamia utekelezaji wa mipango hiyo mipya ya upanuzi, kuongeza ufanisi wa uzalishaji na usambazaji, pamoja na kuhakikisha uwekezaji unaofanywa na SBC unaendelea kuzaa matokeo katika soko la vinywaji linalozidi kuwa na ushindani. 

Anakutana na ushindani wa soko

Katika soko la vinywaji baridi Tanzania, SBC inakabiliana na ushindani kutoka kwa wazalishaji na wasambazaji wengine wa vinywaji, akiwemo Coca-Cola Kwanza, kampuni tanzu ya Coca-Cola Beverages Africa (CCBA).

Coca-Cola Kwanza inaendesha viwanda viwili Tanzania, Dar es Salaam na Mbeya, na inasambaza chapa zikiwemo Coca-Cola, Fanta, Sprite, Schweppes, Dasani na Powerade.

Mbali na washindani hao wa kimataifa, SBC pia inakutana na ushindani kutoka kwa wazalishaji wa ndani, akiwemo A-One Products and Bottlers ya MeTL Group, inayozalisha na kusambaza vinywaji mbalimbali ikiwemo Mo Xtra, Mo Cola, Mo Chungwa na bidhaa za maji kama Masafi na Maisha. 

Kwa Shekhar, jukumu jipya linaweka mezani changamoto ya kuendeleza upanuzi wa uzalishaji na usambazaji, kuongeza upatikanaji wa bidhaa na kuimarisha ushindani wa chapa za SBC katika soko, wakati kampuni ikiendelea kuwekeza katika kuongeza uwezo wa viwanda vyake ili kukidhi mahitaji ya soko. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴 LIVE: WABUNGE WAKIMCHAPA MASWALI MAZITO WAZIRI MKUU BUNGENI

🔴 LIVE: WABUNGE WAKIMCHAPA MASWALI MAZITO WAZIRI MKUU BUNGENI

Nukta TV

CEO, TAB Group: Africa Agri Expo 2026 inakwenda kufungua fursa kimataifa, kilimo cha Tanzania

CEO, TAB Group: Africa Agri Expo 2026 inakwenda kufungua fursa kimataifa, kilimo cha Tanzania

Nukta TV

TANTRADE: Tumieni vifungashio vya "Made in Tanzania"

TANTRADE: Tumieni vifungashio vya "Made in Tanzania"

Nukta TV